Moja ya daraja kubwa ambalo limeondoa usumbufu kwa wakazi wa kata ya majengo na nyasumbi kahama |
KAHAMA
SERIKALI Wilayani hapa Mkoani Shinyanga
imeshauliwa kutumia wakandarasi wa ndani katika shughuli mbalimbali za ujenzi
hali ambayo itaifanya serikali kuwabana wakandarasi hao pindi watakapokwenda
kinyume na makubaliano katika mikataba kuliko wakandarasi wanje ambao
upatikanaji wao unakuwa wa shida mara baada ya kazi.
Aliyasema hayo jana Mkurugenzi wa
Kampuni ya Higen Construction Co Ltd Themistrocles Rwota wakati akizungumza na
wandishi wa habari akiwa katika moja ya majukumu ya ujenzi wa daraja
linalounganisha kata ya kahama mjini na kata ya majengo wilayani hapa.
Alisema kuwa serikali inatakiwa kutumia
wakandarasi wazawa wa ndani katika kuijenga kahama nasio kutumia wakandarasi
kutoka nje nakuongeza kuwa hali hiyo itafanya kila mkandara kufanya kitu kwa
umakini huku akitegemea kupata kazi nyingine pindi atakapomaliza kazi.
Aliendelea kusema kuwa wakandarasi wa
nadani kwa kipindi kirefu wamekuwa hawapatiwi kazi na halmashauri kwa kuogopa
kufanya kazi chini ya kiwango na badala yake frusa hiyo wamelkuwa wakipata
wakandarasi kutoka nchi za jirani nakuongeza kuwa laiti halmashauri
zingelitambua wakandarasi wa ndani ndio wanawoweza kufanya kitu kizuri kyuliko
hata hao.
No comments: