Mtuhumiwa David Faustine Chimomo akiwa anatoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusomewa mashtaka ua uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya bilioni 12.6 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha fedha. Mwanamama Safina Kassim
Rupia na David Faustine Chimomo, wamepandishwa katika kizimba cha mahakama ya
hakimu mkazi kisutu na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia
serikali hasara ya bilioni 12.7 huku wakikwepa kulipa kodi ya kiasi hicho cha
fedha.
Akisoma hati ya mashtaka,
wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi
Godfrey Mwambapa, kuwa, kati ya Julai 11 na Oktoba 28,2015 washtakiwa hao
wakiwa Azam ICD Sokota walitenda makosa hayo.
Imedaiwa, siku hiyo
washtakiwa walisababisha hasara ya Sh 12,618,970,229 kwa mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) kwa kutoa makontena 329 bila ya kulipiwa kodi.
Katuga ameendelea kudai
kuwa,siku hiyo katika bandari Kavu ya Azam ICD iliyopo Sokota katika wilaya ya
Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walisaidia kukwepa kodi ya makontena
329 ambayo kodi yake ilikuwa na thamani ya sh. 12,618,970,229.
Baada ya kusomewa
mashtaka hayo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi ya uhujumu
uchumi hadi Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa wakili
Katuga, Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa
rumande hadi 27,2017 itakapokuja kwa kutajwa.
kwa hisani ya karama kenyuko globu ya jamii
|
No comments: