Wanafunzi watano kati ya 60 wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Katarama, lenye namba za usajili T 431 EHW, kugonga gari dogo aina ya Noah lenye namba T 533 DJP katika Barabara ya Kahama–Masumbwe, mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea wakati wanafunzi hao wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kugongana huko, majeruhi wamepatiwa huduma za awali na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku wengine wakiendelea na uchunguzi wa afya zao.


Tags:
habari
