sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WATENDAJI WAONYWA KUACHA KUWACHANGIA WANANCHI KATIKA KPINDI CHA KILIMO



Na  Mohab Dominick
Kahama
04 nov , 2013.
mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akisisitiza jambo kwa watendaji wa vijiji na kata 


MKUU wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya amewataka Watendaji wa kata na Vijiji kuacha kuwachangisha wananchi michango mbalimbali ya maendeleo katika  kipindi cha kuanzia mwezi wa kumi.

Aliyasema hayo wakati wa Kikao cha Maendeleo ya Wilaya ya Kahama (DCC) na kuongeza kuwa katika kipindi hicho wananchi wanakuwa katika kipindi cha kilimo na kuelekeza nguvu zao katika kupata chakula cha kipindi kijacho.

Mpesya alisema kuwa kama Watendaji hao watawatoza michango katika kipindi hicho Wakulima watakosa fedha za kulimia hali ambayo inaweza kuleta upungufu wa chakula kwa kuwa nguvu zao watakuwa wameelekeza katika michango.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watendaji kujiona kuwa wao ni watu wakubwa katika vituo vya kazi na ni niwatumishi wa Serikali na hivyo kutokubali kuendeshwa kisiasa hali ambyo itawafanya waweze hata kuheshimika katika maeneo ya kazi.

“Ukimwona Mtendaji wa kata yupo sambamba na Diwani wake katika mambo mbalimbali ya kazi ujue kuwa mtendaji huajiamini katika kazi yake anayoifanya na kufanya kutokuwa na maamuzi ya msingi katika kazi anazozifanya”, Alisema Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya.

Pia aliwaasa kuwa na utaratubu wa kusomewa wananchi wao mapato na matumizi kwa kile chocho wananchi wanachochangia katika mambo mbalimbali katika kata zao hali ambayo itawapelekea wananchi kuwa na imani na kazi wanazozifanya.

“Ninawaambia kuwa nyinyi watendaji ni marufuku kuingia katika mradi mwingine bila ya kusoma mapato na matumizi kwa Wananchi unaowaongoza jamii ya sasa ina mwamko mkubwa kwa sasa”, Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Pia alisema kuwa kunapokuwa na jambo lolote la utekelezaji lazima litazamwe kwa makini ili kila mmoja asiweze kuathirika katika shughuli zake anazozifanya hali ambayo itafanya kazi ya utawala bora kufanyika bila ya wasiwasi wowote.

Katika kikao hicho cha maendeleo ya Wilaya mambo mbalimbali yalizungumziwa hasa katika sekta mbalimbali kama vile Elimu maji na Afya huku Kampuni ya Barrick nao wakielimisha washiriki kuhusu kujuhadhari na matumizi ya kemikali  ya Cynide inayotumika katika kukamatia madini ya dhahabu.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply