sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WANAFUNZI WAASWA KUTOKULALAMIKIA WAZAZI



Na  Mohab Dominick
Kahama
Oct 28, 2013.


Mkuu wa shule ya Rocken Hill Alexander kazimiri akipongeza msichana kwa kuongoza masomo yote.

IMEELEZWA kuwa kwa wakati huu Mwanafunzi akishindwa kusoma kwa bidii hakuna haja ya kumlalamikia mzazi kwani wanapata kila kitu tofauti na waliopata Elimu katika kipindi cha nyuma.

Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Anderleck Adamu Rui katika sherehe za mahafali ya tano ya shule hiyo yaliofanyika juzi mjini Kahama na kuongeza kuwa msingi Mkubwa wa maisha ni elimu kwa sasa.

Rui alisema kuwa kwa maisha sasa katika maisha ya sasa sio wanafunzi wote wanapenda shule na kuongeza kuwa wengine ni wakuvumiliana sana kutokana na tabia walizonazo mashuleni kwani wao ndio wanawajua kwa undani zaidi kwa kuwa wanaishi nao kila siku tofauti na wazazi.

Alisema kuwa wanafunzi wa sasa wanapatak kila kitu kutoka kwa wazazi wao tofauti na wale waliokuwa wakisoma katika kipindi cha nyuma hali ambayo wao wanapaswa kuwa kioo cha kwanza na mfano kwa wengine wanaoanza shule.

Aidha Mkuu huyo wa shule aliendelea kusema kuwa suala kubwa kwa mwanafunzi kwa sasa ni mafanikio ya mbeleni na sio kuangalia muda unaendaje bali ni kuangalia yeye kama Mwanafunzi ameutumiaje muda alipokuwa shuleni ili aweze kupata mafanikio.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Anderleck Alexander Kazimiri alisema kuwa wazazi hawana budi kushirikina na walimu katika kuwalea wanafunzi hasa katika masuala makubwa ya maadili na malezi yalio mema hali ambayo italeta mafanikio katika mitihani yao.

Kazimiri alisema kuwa katika maisha ya sasa Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kulalamika tuu bila ya kufanya kazi ikaonekana na kujua kuwa wazazi wapo nyuma yao katika kusimamia malezi yao wanayoyapata tangu wakiwa shuleni hadi wanapomaliza.

“Unajua kwa sasa Vijana wengi wana tabia ya kujua tamthilia za kwenye Runinga kuliko kusoma vitabu huku ikichangiwa na kutokwenda katika maktaba mbalimbali kwa ajili kujikumbusha yale waliokuwa wakifundishwa”, Alisema Alexander Kazimiri.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliojumiuisha wanafunzi 152 Mkuu wa Polisi Mstaafu George Simba aliwataka wanafunzi kudumisha nidhamu ambayo kwa sasa imeshuka kwa kiwango kikubwa kwa wanafunzi.

Pia aliwataka wazazi kuwasaidia vijana hao katika mambo mbalimbali hususani Elimu ili waweze kutimiza ndoto zao walizojiwekea ikiwa ni sambamba na kudhibiti nidhamu wakati wowote watakapokuwa nyumbani wakisubiri matokeo.

Mwisho.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply