HALMASHAURI
mpya ya Wilaya ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ipo mbioni kuanza
kuyapima maeneo ya viwanja vya miji midogo kwa kupitia program za Wanafunzi wa
chuo kikuu cha Ardhi watakapokuwa katika mafunzo kwa vitendo kutokana na
kupungukiwa wataalamu wa idara hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Zabron Donge aliyasema hayo wakati akijibu
swali kutoka kwa Diwani wa Viti maalumu kutoka kata ya Kakola Asha Binde kutaka
kujua kwamba mji huo utapimwa lini baada ya malalamiko mengi kutoka kwa
Wananchi.
Donge
alisema kuwa Halmashauri ya Msalala kwa sasa Haina Wataamu kwa kuweza kupima
maeneo ya mji midogo hususani katika kata ya Kakola badala yake wameo Wanafunzi
kutoka katika chuo kikuu cha Ardhi kuwasaidia katika zoezi hilo pindi
wanapokuwa katika mafunzo ya vitendo.
Alisema
kuwa baada ya kutuma ombi hilo lilikubaliwa na kuongeza kuwa sasa wanasubiri
Wanafunzi hao watakapoanza mafunzo kwa vitendo waje katika Halmashauri ya
Msalala na kupima Viwanja katika mji midogo yote iliyipo katika Halmashauri
hiyo.
Awali
Diwani wa Viti Maalumu kutoka katika kata ya Kakoila Asha Binde alisema kuwa
kwa sasa Wananchi wamekwisha changishwa kiasi cha shilingi 35,000 kwa ajili
upimaji wa Viwanja lakini hadi kufikia hivi sasa bado hawajapimiwa hali
inayowatia wasiwasi.’’
“Kama
Halmashauri imedhamia kuleta Wanafunzi kutoka katika Chuokikuu cha Ardhi kwa
ajili ya zoezi la upimaji ni bora zile fedha walizochangishwa hapo awali kwa
ajili ya zoezi wakarudishiwa ili waweze kufanyia mambo mengine”, Alisema Asha
Binde.
Aidha
Diwani huyo alilaani kitendo cha kiongozi mmoja kutoka katika kata hiyo
kuwachangishaw Wananchi hao kiasi cha shilingi 35,000 kwa ajili ya umimaji wa
viwanja badala ya shilingi 30,000 hali ambayo ilimfanya kupata kiasi cha zaidi
ya shingi milioni moja hali ambayo ni wizi wa kauminika.
“Huyo
kiongozi wa Serikali aliwachangiasha Wananchi shilingi 35,000 badala ya
shilingi 30,000 huku akiwaibia shilingi 5,000 kwa kila Mwananchi nab ado anafanya
kazi katika Halmashauri ya Ushetu baada ya kukimbia Halmashauri ya Masalala
tunakuomba Mkurugenzi Mtumishi huyo aweze kuwajibishwa ili arudishe fedha hizo”,
Alisema Diwani huyo.
mwisho
No comments: