KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) imesema kuwa itaendelea kuungamkono jitihada zinazofanywa
na Serikali katika kupambana na winmbi la majangili wanaouwa Tembo hapa nchini
hasa kwa kupitia bia yake ya Ndovu.
Hayo
yalisemwa juzi na Afisa Tarafa ya Msalala Addy Mtaule wakati wa sherehe
iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ya bia iliyojumuisha wadau mbalimbali wa Kampuni
hiyo na wauzaji wa bia katika mji wa Kahama kwa ujumla .
Mtaule
aliyasema hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambaye
alikuwa Mgeni Mgeni Rasmi katika sherehe hiyo na kuongeza kuwa Serikali itakuwa
bega kwa bega n a Kampuni hiyo
Alisema
kuwa kwa sasa hapa nchini kumekuwa na wimbi kubwa la mauwaji ya Mnyama Tembo
huku majangili hao wakichukua Pembe zake na kwenda kuuza katika nchi mbalimbali
kwa lengo la kutafuta utajiri wa haraka.
Awali
akitoa Salamu za TBL Meneja Mauzo kanda ya ziwa Sylivester Syzya alisema kuwa
lengo kubwa la kufanya sherehe hiyo ni kufahamiana na kuongea mambo mbalimbali
yanayohusu biashara hususani zile bidhaa zinazotengenezwa na Kampuni hiyo
pamoja na wateja wao.
“Tuna
muda mwingi hatujawakutanishja wateja wetu kwa lengo la kufahamiana na
kuzungumza kuhusu nini tufanye sisi kama Kampuni ya biasha na ni nini
kimepungua ili tuweze kuboresha hasa katika bia ya Ndovu”, Alisema Syzya Meneja
mauzo kanda ya ziwa.
Aidha
Meneja huyo alisema kuwa Kampuni hiyo itaendelea katika kuwajali Wateja wake
katika mambo mbalimbali ya kuboresha biashara zao ili waweze kutimiza malengo yao
la kuwa na mitaji mikubwa itakayowasadia katika kupanua wigo wa biashara.
mwisho
No comments: