sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WATAKIWA KUWACHANGIA WAJASILIMALI WADOGO.

 Mc mwl tandise  wa shughuli ya sherehe ya uzinduzi na harambee ya chama cha ushirika cha wajasiliamali wa bulyanhulu
 Mgeni rasmini mkuu wa wilaya kahama benson mpesya mwenye kipasauti akitoa neno kwa wageni walikwa
 Mwenye miwani ni mwenyekiti wa becos  makoba akiteta jambo na mkurungezi wa halmashauri ya msalala patrick charles kwenye harambee ya wajasiliamali wadogo wadogo
 Mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya akitoa jambo
 Moja wa kinamama wa kikundi cha wajasiliamali wakitoa mchango wake wakati wa harambee hiyo
 Baadhi ya viongozi wa becos wakiwa na mkuk wa wilaya ya kahama mwenye tai na mkurungezi wa halmashauri ya msalala wakati wa harambee
 Baadhi ya wageni walikwa

 Mwenyekiti wa becos makoba akitoa neno la shukurani kwa wageni walikwa

 katibu wa becos akishukuru kwa michango yao

 Mkuu karibu sana hayo ni maneno ya mc kwa kwa mkuu wa wilaya ya kahama mwenye tai nyeupe
                                      



Na  Mohab Dominick
Kahama
Julay 29, 2014.

WANANCHI pamoja na Wafanyabiashara wenye uwezo wa kifedha waametakiwa kujitoa katika kuwasaidia wananchi Wajasiliamali wadogo ambao hawana uwezo wa kuwa na mitaji mikubwa ya kufanya Biashara ili kuwainua kiuchumi na kuweza kumudu maisha.

Katibu wa Chama cha Wajasiliamali wadogo kutoka katika kata ya Bulyanhulu (BECOS) Mwita Bhoke aliyasema hayo juzi wakati akiongea na blog hii muda mfupi baada ya kufanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili kutunisha mfuko wa chama hicho.

Bhoke alisema kuwa lengo la kuchangia harambee hiyo ni kutunisha mfuko wa chama hicho kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuweza kuanzisha ushirika ambao ungeweza kuwasaidia wajasiliamali wadogo katika kata ya Bulyanhulu.

Alisema kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto kubwa  ya kutokuwa na mitaji pamoja na masoko  ya bidhaa na huduma katika jitihada za kujikwamua  katika umasikini uliopo kwa wajasiliamali hao.

Katibu huyo aliendelea kusema kuwa chama hicho kilianzishwa mwaka 2014 na kuongeza kuwa  wamepata wakati mgumu  kwa kufanya shughuli za ujasiliamali kutokana na  kutokuwa na mitaji ya kutosha pamoja na mafunzo na zana bora pamoja na masoko.

Pia aliendelea kusema kuwa nje ya umoja huo pia wamekosa fursa nyingi  za kiuchumi  kwa sababu ya kutoaminiwa  kwa mtu mmoja mmoja  na wadau wa kiuchumi akitolea mfano wa Serikali pamoja na taasisi mbalimbali za maendeleo wamekuwa wakihamasisha wananchi kujiunga katika vikundi  ili wapewe mafunzo.

Katibu huyo alisema kuwa katika kataya Bulyanhulu kihistoria kuna shughuli za uchimbaji mdogomdogo unaoendelea  tangu miaka ya 1990 huku ongezeko kubwa la watu likikadiriwa kuwa ni jumla ya watu 50,000 kwa Vijiji sita hali ambayo wakipata angalau mitaji ya kufanya biashara ndogo ndogo watakuwa wamejikomboa kiuchumi.

Katika harambee hiyo iliyokuwa na lengo la kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 lakini jumla ya shilingi milioni 16 zilichangishwa huku ikiwa ni pamoja  na ahadi mbalimbali kutoka kwa wafadhili pamoja na makampuni mbalimbali yaliopo mjini Kahama.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply