sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » KIJANA MOJA ANUSHURIKA KIFO NA MWINGINE AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO. Kijana moja ambaye ajafahamika makazi yake wala jina lake amenushurika kifo maeneo ya kata ya  mwendakulima mjini kahama.hapa yupo hoi baada ya wasamalia wema kumuokoa na kipingo kikali toka kwa mwananchi wenye hasira kali .


 Hapa ni baadhi ya mwananchi wakijalibu kumtambua kijana huyo.
 Baada ya kufikishwa hospital ya wilaya ya kahama kwa matibabu ana baada ya wasamaria wema wakimsaidia nesi kumpeleka kwa dakitali kwa huduma .
 Nes nisaindieni jaamani nipo pekee yangu ndiyo maneno ya nes naosema na  kumuweka katika kiti cha wangonjwa .
 Njamaaa muinueni huko tumuweke kwenye kiti kwa ajili ya huduma hospitali ya wilaya ya kahama
 jaamani hajakaa vizuri mshikilieni vizuri kwanza
 Haya twendeni vizuri sasa angali huko kwako ana nguvu huyu mtu hunaona  halivyokaaa
 Twendeni sasa
 Jamaani nakufa hayo ni maneno ya huyo kijana hakisema kwa tabu sana
 Hoi kijana wa watu
 Haya kaa vizuri kaka umekwisha fika hapa hospitali
 Haya twende sasa
Na  Mohab Dominick
Kahama
Agosti 21,2014

 
Kijana mmoja anayekadiriwa kwa na umri wa miaka 30-32 ambaye hajafahamika majina wala makazi yake ameuawa kwa  kupigwa mawe, kisha kuchomwa moto na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, baada ya kumtuhumu kutapeli pikipiki.

Tukio hilo limetokea jana  majira ya saa tano asubuhi katika mtaa wa Nyihogo, eneo la Mnazi Mmoja, Barabara ya Tabora Karibu na Ofisi za halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

 Mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu inadaiwa alikodisha Pikipiki hiyo  zaidi ya Miezi mitatu iliyopita katika eneo la Maegesho ya Daladala za Pikipiki katika Lango kuu la hospital ya Wilaya hiyo.

Aidha Mmiliki wa Pikipiki hiyo ambaye hajafahamika mara moja wala namba ya  pikipiki, inadaiwa alimkamata  maeneo ya mtaa wa Shunu Kata ya Nyahanga ambapo aliamua kumpeleka katika kituo cha polisi  akiwa amemfunga kamba.

 Baada ya wananchi kuona mtuhumiwa amefungwa kamba ndipo wakamuuliza mmiliki huyo ambaye aliwaeleza, na ghafla wananchi wakaanza kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma Moto.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga Justus kamugisha Amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa ni kweli tukio hilo limetoka jana majira ya asubuhi saa 5 kijana moja ambaye jina lake alikuweza kufahamika mara moja alikuwa amekamatwa na mwanachi moja ambapo alikuwa ametoloka na pikipiki yake maeneo ya nyahanga wilayani kahama .

Aidha kamanda kamugisha alizidi kuelezea kuwa pamoja na tukio hilo kutokea kwa kijana huyo  jeshi la polisi linawatafuta watu wote walifanya mauji hayo

 Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply