sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA WATOTO 3 WAKAMATWA KAHAMA

 picha wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji wilaya ya kahama baada ya kukamatwa kituo cha basi
 Afisa wa uhamiaji akichukuwa maelezo kwa muhamiaji haramut tengemea Benjamini  ofisi za uhamiaji
 IRene mkazi wa ngara ambaye moja wa tanzania ambaye anajiushisha na kukaa na wahamiaji haramu na mtoto khadija 8 miaka  ambaye ni Raia wa Burundi anayefanya naye kazi kwake.
 Baadhi ya wahamiaji wakiwa chini ya ulinzi katika ofisi za uhamiaji kahama baada ya kukamatwa.
 Mtoto khadija akiwa na mtoto wa Ireni stephen  ambaye amembeba kwa ajili ya kumlea mtoto huyo.
 Irene akiwa na watoto wake wawili na mfanyakazi wake wa watoto wake khadija ofisi ya uhamiaji kahama kwa mahojiano.
 Irene akiwa na afisa wa kike ofisi za uhamiaji kahama na watoto wake baada ya kukamatwa kituo cha mabasi.
 Irene akihojiwa na kamishina wa uhamiaji Zakaria Misana ofisi kwake kwa kosa la kukaa na mtoto wa miaka 8 kumfanyisha kazi kinyume na sheria
                         kamishina wa uhamiaji zakari misana akiongea na waandishi wa habari ambao wapo picha juu ya wahamiaji haramu ofisini kwake .
 Wahamiaji haramu wakiwa ofisi za uhamiaji kwa kosa la kuingia nchini bila kibali


Afisa wa uhamiaji akifanya mahojiano na moja wa wahamiaji haramu ofisi za uhamiaji .

Na  Mohab Dominick
KAHAMA
August 26, 2014.

Wahamiaji haramu kumi na watoto watatu wamekamatwa wilayani kahama mkoani shinyanga wakiwa wakielekea mkoani tabora kwenye mashamba ya tumbaku kwa ajili ya kilimo.

Haya aliyesema hayo jana  kamishana wa Uhamiaji Wilaya ya Kahama Zakari misana wakati akizungumza na redio kyela fm ofisini kwake ambapo alisema kuwa wahamiaji hao walikamatwa katika kituo cha mabasi wakati wakimsubiri mwenyeji wao ili kuwapeleka mkoani tabora.

Alisema kuwa wahamiaji hao ambao ni Rai wa nchi jamhuri ya Burundi waliangizwa na mkazi moja wa Tabora ambaye aliyejulikana  kwa jina moja la shabani,ambapo baada ya kukamatwa na kupata taarifa ndipo wenyeji wao walipokimbia kutojulikana.

Misana aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Emily Havyarinana(33),Habimana paschal(45),masabo Tadei( 34),Bahati leopoo( 42),Niondeze John(24),Emmanuel mathayo( 21),Tegemea Benjamini( 23) mkazi wa chivu ,joseph Elias (12), ,Laneck wilford (17),Estar John (18) raia wa Burundi pamoja na  Irene stephe(20)raia wa Tanzania  mkazi wa ngara.

Aidha Misana alisema kuwa walikuwa wanakwenda Mkoani Tabora katika kijiji cha Isakamleme kwa ajili ya shughuli za kuvuna mahindi, kuchambua Tumbaku pamoja na kuvuna  mpunga.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Irene Staphano ameajili mtoto mwenye umri wa miaka(8) aliyejulikana kwa jina moja la Khadija mkazi wa Burundi jambo ambalo ni kosa kuajili mtoto mdogo ambapo ni kinyume cha sheria ya jamhuri ya Muungano waTanzania.
 
Misana alisema  miezi kama hii katika mikoa ya mipakani kumekuwa na tatizo la wahamiaji haramu wanaokimbilia mikoa ya kagera,Tabora pamoja na shinyanga, ambapo wilaya ya kahama imejipanga vyema katika kamati ya ulinzi ili kudhibiti jambo hilo.

Misana aliwataka watendaji wa kata na vijiji  vilivyopo mipakani kushirikiana na wananchi kudhibiti matatizo ya wahamiaji hao ambapo amesema kuwa atakayebainika kuishi na raia ambaye sio raia ya Tanznia atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ambapo alisema kuwa wahamiaji hao watachukuliwa hatua za kisheria baada ya kuingia nchini bila kibali hivyo watafikishwa mahakamani wilayani humo ili  kujibu kesi inayowakabili.

Mwisho



 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply