sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Baba Mzazi amuzuia mtoto wake wa kike kufanya mtihiani wa kuhitimu Elimu ya msingi



Na Mohab Dominick
Sept 10,2014
Geita-Bukombe.

  MWANAFUNZI  wa kike Shule ya msingi Ihulike Iliyoko kata ya Ushirombo Wilayani Bukombe Mkoani Geita amezuiwa na baba yake asishiriki kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi unaondelea asije akafauru ikzuia mpango wake wa kumuozesha ili apate posa ama mahari.
 
Afisa Elimu msingi Wilaya ya Bukombe Shadrack Kabanga amesema kuwa wmepokea taarifa toka kwa wasamalia wema ambao walimtumia ujumbe kwa sms kuhusu mzazi wa mwanafunzi Shija Athanas Lusesa ambaye ni athanas Lusesa mkazi wa kijiji cha Ihulike kata ya ushirombo kuwa amemzuia binti yake huyo asiende kufanya mtihani na kweli  hakufanya mitihani yote ya septemba 10 .
Baada ya kupokea taarifa hizo jioni majira ya saa kumi alichukuwa hatua ya kwenda shuleni Ihulike kujiridhisha na kukuta kweli mwanafunzi huyo hakuwepo shuleni kushiriki na wenzake kufanya mtihani ingawa alikuwa amejiandaa na dawati la kufanyia mtihani.

Afisa elimu  amesema baada ya kujiridhisha amechukua hatua ya kwenda polisi  kuchukua Askali na kumkamata mzazi huyo na hadi sasa yuko mikononi mwa polisi baada ya mitihani kumalizika watamfikisha mahakamani kujibu mashitaka.

Aidha Kabanga amesema kuwa mwanfunzi Shija Athanas atafanya mitihani iliyosalia akishirikiana na wenzake kwa kuwa yeye yuko tayari kufanya mtihani.

Afisa elimu Kabanga ametoa wito kwa wazazi wote wenye tabia kama hiyo waache mara moja kwani serikali imejipanga kukabiliana na wazazi ama watu wanaotaka kuwazuia watoto wa kike kupata elimu ya msingi na sekondari.

Amesema Athans Lusesa atakuwa wa mfano kwa  wazazi wengine wenye tabia kama hizi hasa sehemu za wafugaji kwani limekuwa ni jambo la kawaida kwa wazazi kuwaachisha masomo watoto wa kike na kwenda kuwaoza  ili kujipatia Mali.

Aidha mkuu wa wilaya ya Bukombe amani mwenegoha amelaani vikali kitendo hicho kilichofanya namzazi huyo kwa lengo la kujipatia mali nakusema”sisi kama serikali ya wilaya naserikali kuu kwa ujumla wake inakemea vikali vitendo vya wazazi kama hawa wanaozuia jitihada za serikali kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu’

Akifafanua zaidi mkuu wa wilaya amesema kuwa serikali haitavumilia vitendo kama hivi hasa katika maeneo ya wafugaji  ,wachimba madini watu wanaohamahama ovyo ili kuharibu utaratibu wa elimu hasa maeneo ya ufugaji.

Amesema kuwa kwa kuwa mwanafunzi Shija Athanas ameshindwa kufanya mitihani ya awali basi serikali itahakikisha atafanya mitihani yake yote baada ya kutengewa siku yake pekee na huku yeye babayake mzazi aliyesababisha hayo atashikiliwa na hatimaye kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumzuia mwanafunzi  kufanya mtihani wake wa kuhitimu Elimu ya msingi.

Jumla ya wanafunzi 3731 wilayni Bukombe mkoani Geita wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu ambayo iliayoanza tarehe 10 hadi 11 mwezi septemba.

MWISHO

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply