sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » CCM SHINYANGA YAWATAKA WATENDAJI WAKE KUDHIBITI MAUWAJI YA VIKONGWE SHINYANGA.

 Mlemavu wa ngozi kabula akiwa nje ya mahakama ya wilaya ya kahama akiwa na mwalimu wake na baadhi ya wazazi wake siku ya kesi yake ya kukatwa mkono na watu mwenye imani za kishirikina.
Vick mtetema akiwa na mlemavu wa ngozi mjini shinyanga katika ziara yake ya kuangalia walemavu wa ngozi na kuwapa faraja .
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa  shinyanga khamis mgeja juu ya  mauaji ya vikongwe wakati wa ziara yake halmashauri ya shinyanga .

Na Mohab Dominick
Shinyanga
Sept 4, 2014.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga kimewaagiza viongozi na watendaji wote wa serikali ya mkoani humo kuchukua mara moja hatua za kukabiliana na wimbi la mauaji ya vikongwe,  watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) na ubakwaji wa watoto matukio yanayochafua na kuharibu sifa ya mkoa huo.

Agizo hilo limetolewa juzi na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja alipokuwa akizungumza na viongozi na watendaji wa serikali, halmashauri ya manispaa ya Shinyanga na baadhi ya madiwani katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku mbili wilayani Shinyanga.

Mgeja alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi akielezea tukio la wiki mbili zilizopita ambapo mtoto mwenye umri wa miaka tisa mkazi wa kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga alibakwa hadi kufa na watu wasiojulikana kisha walimtoboa macho yake yote mawili.

Pia ilielezwa kuwepo kwa ongezeko la mauaji ya kikatili dhidi ya wanawake vikongwe katika siku za hivi karibuni mkoani humo hali ambayo imesababisha wakazi wengi wa mkoa huo wakiwemo wazazi na walezi wenye watoto wa kike kuishi maisha ya wasiwasi kwa kutokufahamu lini watafikwa na majanga hayo.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa huyo wa CCM aliwataka viongozi wote wa serikali na halmashauri za wilaya wahakikishe wanaweka mikakati madhubuti itakayokuwa endelevu jinsi ya kukabiliana na matukio hayo ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakwaji wa watoto wadogo kwa kuyazuia mapema badala ya kusubiri kuyashughulikia yanapokuwa yametokea.

“Chama Cha Mapinduzi tunasikitishwa sana na matukio haya kwa kweli yanachafua sura ya mkoa wetu, sasa tunakuagizeni viongozi na watendaji wote wa serikali na wale wa serikali za mitaa hakikisheni kuanzia sasa mnaweka mikakati endelevu ya kukomesha mauaji na vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani mwetu, acheni tabia ya kusubiri kushughulikia matukio,”

“Suala la ulinzi na usalama limesisitizwa sana ndani ya ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2010 – 2015, hivyo ni muhimu wenzetu ambao ndiyo watekelezaji muhakikishe wananchi wanalindwa ili waishi kwa amani na utulivu hii imeelezwa ndani ya ibara ya 206 hadi 208 ambamo imeelezwa wazi kuhusu ulinzi kwa makundi maalumu,” alieleza Mgeja.

Alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kushirikiana na viongozi na watendaji wa serikali katika kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili badala ya kuliacha jukumu hilo mikononi mwa vyombo vya dola pekee na kwamba kila mmoja ni mlinzi katika eneo lake hivyo ni rahisi zaidi kwa wananchi kuwatambua watu wote wanaojihusisha na ukatili huo wa kinyama.

“Naamini tukiweka mikakati endelevu katika ngazi zote, mkoa, wilaya, kata hadi vijijini na tuwe na agenda ya kudumu katika vikao vyetu tujadiliane jinsi ya kupamba na janga hili ambalo ni janga la mkoa, tusiwe na tabia ya kushughulikia matatizo haya kwa mfano wa zimamoto, yaani tunakaa tukisubiri yatokee ndipo tunaanza kuhangaika, hapana tuache mtindo huu,” alieleza.


Mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply