sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU KAHAMA WAMEOMBWA KUTUMIA FAIDA WANAYOIPATA KUTOKANA NA ZAO HILO



Na  Mohab Dominick
    KAHAMA
  Sept  4,2014

Wakulima wa  zao la Tumbaku wilayani Kahama Mkoani shinyanga wametakiwa kutumia faida wanayoipata kutokana na zao hilo kujiimarisha kiuchumi ikiwemo kujenga nyumba  bora na za  kisasa na kusomesha  hasa  watoto wa kike shule.

Hayo yalisemwa jana na Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Ushetu Deogratius Rugangila wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Bodi ya Ushirika katika chama cha Msingi Tembo (Amcs LTD) Kata ya Bulungwa.

Alisema kuwa  mara nyingi wakulima wa zao la Tumbaku wameendelea kuwa katika hali ya umasikini kutokana na  kuendekeza Starehe  pindi wanapokwenda kuchukua fedha katika mabenki  na kujikuta wakibakiza fedha kwaajili ya mtaji wa maandalizi ya msimu mpya.

Rugangila aliwataka wakulima wa zao hilo kuwa na ushindani wa Kiuchumi katika kubadilisha maisha ya familia zao ili kuleta mabadiliko ya maendeleo haraka zaidi katika maeneo mengi.

Aidha aliwataka kuwa wananchama wa Tembo Kuachana na makundi ya Uchaguzi na badala yake wajikite kuimarisha chama chao na kwamba viongozi wa bodi kuwatumikia ipasavyo wanachama ikiwa ni pamoja na kushirikishana ndani ya chama.

Alisema kuwa  matatizo ya wanachama yanamalizwa ndani ya Chama chao na si kuyapeleka Nje kwani hali hiyo itasababisha kuwepo na Makundi na kamba kila mwanachama kuwa makini na mali za chama ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mwenyekiti amechaguliwa Julius Nkomangi ambaye alipata kura 221 dhidi ya kura 89 za Furaha Lukelelwa nafasi ya Makamu mwenyekiti imekwenda kwa Joseph Maige kwa kura 247 ambaye alimshinda mpinzani wake wa karibu  Hamis Manyansura aliyepata kura 60.

Aidha Masanja Lupili alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Tembo katika bodi hiyo huku wajumbe ni Furaha Lukelelwa,Charles Makoye, Richard Msafiri,Hamis Manyansura, Eliac Juma, Kazyoba Charles na Marko Bundala.
mwisho 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply