sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » MBOWE HALETA KIZANZA DAR

 Hapa ni majadiliano hawa askari  jamaa wako wape hayo ni maneno ya polisi kuhangalia hali ya usalama jijini

Mwandishi wa habari Badi akilia baada ya kushambuliwa na Polisi,huyu ni moja ya waandishi walioshambuliwa

 Ili kuzibidhibiti hali ya ulinzi jiji dar polisi waliweka ulinzi mkali sana kila eneo la jijini kama polisi wanavyoneka na mbwa zao barabarani
 TWende huku tulia hii ndiyo hali ilivyokuwa katika jiji la dar
 Wewe tulia hapo hupo chini ya ulinzi


 Hivi ndiyo hali hilivyokuwa jiji ulinzi mkali kuliko maelezo .

Kuna taarifa kuwa mwaandishi wa habari wa IPP Media kapigwa na jeshi la polisi alipokuwa ameenda kuripoti matukio yaliyokuwa yanaendelea baada ya mwenyekiti wa CHADEMA Mhe, Mbowe alipoenda kuitikia wito wa jeshi hilo la polisi.

Habari zinasema kuwa  baada ya Mbowe na wanasheria kuingia ndani polisi walianza kupiga kila aliyekuwa eneo la tukio bila kujali ni nani ndipo alipojikuta mwandishi huyo akipigwa mpaka kupoteza fahamu.

Imeelezwa kuwa waandishi wengi wa habari wameumia vibaya kutokana na kukimbizwa na mbwa wa polisi huku wengine wakiumwa na mbwa hao.

Waandishi wa habari wameshindwa kutimiza wajibu wao kwa kuzuiwa na polisi ambao wameshindwa kutambua uwepo wa waandishi wa habari,Je Uhuru wa vyombo vya habari uko wapi Tanzania? na kama waandishi wa habari wameanza kuumizwa mapemaa kabisa kabla hata kampeni za uchaguzi hazijaanza,Sijui uchaguzi ukifika hali itakuwaje!!

Ikumbukwe kuwa Mwaka jana mwandishi wa habari Daud Mwangosi aliuawa kikatili kwa amri ya RPC (Kamuhanda) wa Iringa wa wakati huo ambaye baada ya kutimiza azima yake hiyo alipandishwa cheo.

Mami ya watu leo wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi  nchini, jijini Dar es Salaam kuhusiana na kauli yake aliyotoa Septemba 14 mwaka huu,juu ya kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.

Kilichofuata ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa umbali wa mita 200 ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao waliumia na kupoteza zana zao za kazi

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply