sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MME AKATA NYETI ZA MKEWE NA KUPELEKA KWA SANGOMA.


Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti)Akiwa wodi  katika hospital ya mkoa wa  Tabora .

 MME AKATA NYETI ZA MKEWE NA KUPELEKA KWA SANGOMA.

 Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliyekatwa sehemu zake za siri (nyeti) na mumewe anayefahamika kwa jina moja la Mashaka.

 Wito umetolewa kwa wananchi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu pindi vinapotokea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo baya, mama huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete ambapo anadaiwa kukutwa na kisanga hicho hivi karibuni.

Mwanamke huyo anadai kujeruhiwa na mumewe usiku wakati wakiwa wamelala nyumbani kwao Mtaa wa Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora.

 Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu akiwa wodini kwenye hospitali hiyo akiwa na maumivu makali, mama huyo alikuwa na haya ya kusema:

“Siku ya tukio, nakumbuka mume wangu alikwenda kutembea, aliporejea nyumbani alifuatana na mtu mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji.

“Walipofika nyumbani aliniambia yupo na mganga wa kienyeji ambaye alikuwa akitafuta viungo vya sehemu za siri za mwanamke akiwa na fedha milioni tano.  Mimi nilikataa baada ya kunishawishi lakini usiku nilipokuwa nimelala, mume wangu alinikata huku akiniamuru nisipige kelele kwa kuwa alikuwa ameshapatana bei na kwamba ulikuwa ni utajiri mkubwa.”

Alisema baada ya tukio hilo alijikuta amelazwa hospitalini hapo hivyo hajui kama mumewe huyo alishakamatwa au la.

 Kwa mujibu wa majirani zao, Mtaa wa Kazaroho, lilikuwa ni tukio la kutisha kwani wasamaria wema ndiyo waliomkimbiza mama huyo hospitalini ili kuokoa uhai wake.

Majirani hao walimtaka Waziri wa Maendeleo ya Wanawake Jinsia na Watoto, Sophia Simba kufanya kazi ya ziada ili sheria ichukue mkondo wake ili kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyoshamiri kwa kasi nchini.

 Mmoja wa madaktari hospitalini hapo ambaye hakutaka kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, mama huyo alifikishwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini baadaye alipata nafuu hivyo anaendelea vizuri na matibabu. Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Suzane Kaganda aliyehamishiwa mkoani hapa hivi karibuni hazikuzaa matunda hivyo zinaendelea

 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply