sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » TASAF YAVIPONGEZA VYOMBO VYA HABARI KWA MCHANGO WAKE

 Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Tasaf Zuhura Mdungi Akitoa maelenzo kwenye kikao kazi cha waratibu wa mpango ,Maafisa ushauri na usimamizi Na Waandishi wa Habari wa mikoa ya Geita ,Kagera na Geita
 Baadhi ya Waandishi wa kiteingo cha habari cha Tasaf kinagho Banduka na Victor Manyai.
 Baadhi ya Waandishi wakisikiliza maanda toka kwa kiongozi wa Tasaf Taifa.
 Hivi ndiyo hali halisi ya kikao kazi kwa waandishi wa habari kama huyu dada halivyochoka na kazi ya kusikiliza maada .
 Waandishi wakiwa makini kusikiliza Maada ya kikao kazi jiji mwanza.
 Umakini tunasikiliza
 Baadhi ya Waandishi wa habari  na viongozi wa Tasaf Taifa na  mkoa wa shinyanga wakiwa katika picha  pamoja .
 Waandishi wa Habari wakisikiliza .
 Muandishi wa gazeti la majira Mkoa wa shinyanga Selemani Abeid akisikiliza maada ya kikao kazi  cha Tasaf jiji mwanza .
 Waandishi wakiwa makini
 Wandishi wakifatilia kwa makini
 Umakini kwa kusikiliza 

VYOMBO vya habari nchini vimetajwa kuwa na mchango mkubwa katika ufanikishaji wa Mpango wa kuzinusuru kaya maskini nchini unaotekelezwa kupitia TASAF awamu ya tatu.

Hali hiyo imeelezwa na mkurugenzi mkuu wa TASAF nchini, Ladislaus Mwamanga katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Ukaguzi, Christopher Sanga katika kikao cha kazi cha watendaji wa TASAF na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Shinyanga, Geita na Kagera kinachofanyika jijini Mwanza.

Katika hotuba yake Mwamanga alisema vyombo vya habari vinategemewa kuwa na mchango mkubwa katika kuihabarisha jamii ili iweze kuelewe malengo mahususi ya kuanzishwa kwa mpango wa kuzinusuru kaya maskini nchini na kwamba iwapo jamii itapata habari sahihi itaweza kuutekeleza vyema mpango huo.

“Kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari, tangu awali TASAF imekuwa ikivishirikisha vyombo hivyo katika utoaji wa elimu ya shughuli mbalimbali zinazotekelezwa ili walengwa waweze kufahamu shughuli zetu, lengo la kuwashirikisha ni kuhakikisha mnafikisha ujumbe sahihi kwa wananchi,”

“Pamoja na kwamba pamekuwepo na upotoshwaji kuhusu shughuli za TASAF, hususan kuhusiana na utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini, baadhi ya ujumbe unaowasilishwa na baadhi ya vyombo vya habari siyo sahihi,”

“Hivyo TASAF tumeona haja ya kuandaa vikao hivi vya kazi kwa nchi nzima ili wote tuweze kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mpango kwa lengo la kuhakikisha tunafikisha ujumbe sahihi kwa wananchi,” ilieleza sehemu ya hotuba ya mkurugenzi huyo.

Alisema ushirikishwaji wa jamii na wadau mbalimbali ni moja ya misingi ya TASAF, hivyo anatarajia kikao hicho cha kazi kilichowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari kitaimarisha ushirikiano kati ya wanahabari na TASAF.
 
Mkurugenzi huyo alisema TASAF ni chombo cha serikali na hakifungamani na chama chochote cha kisiasa au kidini na kwamba lengo kuu la mpango unaondelea hivi sasa nchini ni kuzinusuru kaya maskini kwa kujenga raslimali watu ya baadaye kwa kuziwezesha kaya hizo katika lishe, afya na elimu hasa kwa watoto.

“Awali katika awamu zilizotangulia, TASAF iliweka msisitizo mkubwa katika utekelezaji wa miradi kama ujenzi wa shule, zahanati na maji kwa lengo la kuhakikisha kaya maskini zinanufaika na huduma hizo muhimu, lakini tathimini zilionesha kaya hizo hazifaidiki kwa kwa kiwango kikubwa na huduma hizo,”

“Baadhi ya watoto kutoka katika kaya maskini walilazimika kufanya vibarua na biashara ndogo ndogo kama kuuza karanga badala ya kuwa shuleni na baadhi ya kaya hizo hazikuweza kuwapeleka watoto wadogo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya chanjo na kufuatilia afya zao,” alieleza Mwamanga.

Alisema mpaka hivi sasa tayari kuna mafanikio chanya yaliyoanza kuonekana kwa walengwa wamelionufaika na ruzuku iliyotolewa hususan katika nyanja za elimu, afya, lishe, makazi na hata kuweza kuwa na shughuli za uzalishaji mali kwenye maeneo yao na tayari kiasi cha shilingi bilioni 49 zimetolewa kwa walengwa wa mpango huo nchini kote.


"Mafanikio haya yaliyopatikana yanapaswa kutangazwa ikiwa ni pamoja na changamoto zake ili kuwezesha mfuko kuboresha zaidi huduma hizi huku walengwa nao wakielimishwa zaidi namna ya kutumia fursa hii katika kujikomboa kutoka kwenye dimbwi la umaskini," alieleza Mwamanga.



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply