sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WASANII WA BONGO MOVIE ,WATANGAZA KUTEMBEA NCHI NZIMA KWA BAJAJ KUMUUNGA MKONO TINGA TINGA






Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.





Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.




Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.








Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda nafasi ya Urais.




Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano




Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.





Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.




Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.




Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.




Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda




Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana




wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.




Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.




Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.




Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
 

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply