sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MKE WA MHESHIMIWA LOWASSA AKATAA UBUNGE CHADEMA...ADAI ATAKOMAA NA AKINA MAMA NJE YA BUNGE


 Mama Regina Lowassa.

Mke wa aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mama Regina Lowassa.




 Mama Regina Lowassa Akiwa katika moja ya Mikutano ya kampeni Mkoa wa kilimanjaro jimbo la hai
DAR

Ameikataa kwa nia njema nafasi aliyopewa ya kuwa mbunge wa viti maalum kupitia chama hicho. 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilitangaza mgawanyo wa viti maalum jana ulioonyesha kuwa Chadema imevuna viti 36, ikiwa ni ongezeko kubwa lililotokana na kufanya vizuri zaidi katika majimbo kulinganisha na uchaguzi wa mwaka 2010 wakati walipopata idadi ya viti maalum isiyokaribia 30. 

Taarifa iliyopatikana jijini Dar es Salaam jana ilieleza kuwa mama Lowassa ambaye alifanya kazi kubwa ya kupigania mafanikio ya Chadema wakati wa kampeni, ameikataa kwa nia njema nafasi hiyo aliyopewa na kamati Kuu ya Chadema. 

Ilielezwa kuwa Mama Regina aliipokea kwa heshima nafasi hiyo, lakini anaamini bado anao uwezo wa kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya bunge. 

"Naishukuru kamati kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na ninaithamini sana. Lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea kina mama mabadiliko na kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," Mama Lowassa alikaririwa akisema. 

Kamati Kuu ya Chadema iliamua kumtunuku nafasi ya ubunge viti maalum kutokana na mchango mkubwa alioutoa wakati wa kampeni ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia upatikanaji wa kura nyingi kwenye majimbo ya uchaguzi na mwishowe chama hicho kikatangaziwa na NEC kupata nafasi 36 za viti maalum.



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply