Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,
PC Asha Adam, akiwasisitiza abiria kufunga mikanda iliyopo kwenye viti
walivyoketi muda wote wa safari muda mfupi kabla ya magari kuondoka
katika kituo Kikuu cha mabasi ya abiria Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo
Novemba 10, 2015 kama hatua ya kudhibiti majeraha na vifo vitokanavyo na ajali
za barabarani, kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka,
Askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Samwi(kushoto), na PC Elisante Bura(kulia),
wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani, kutekeleza mkakati wa
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea
kipindi cha mwisho wa mwaka.Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya
magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam
kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania .
Askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Swami(aliyeko chini ya uvungu wa gari),
akikagua moja ya magari yanayojiandaa kuelekea mikoani, zoezi ambalo
limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuanza kuondoka katika kituo Kikuu cha
Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante
Bura. Hatua hii ya Jeshi la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali
kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka,.
Askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani,Sajenti Jackson Mafuru (kulia), na PC Elisante Bura(kushoto),
wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani. zoezi hili ambalo
limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu
cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam, ni moja ya hatua ya Jeshi la Polisi
kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha
mwisho wa mwaka,.
Askari wa Kikosi cha Usalama
Barabarani,Koplo Abdallah Bwasi akikagua moja ya magari yanayofanya
safari zake nje ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi kabla ya magari
kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam.Hatua hii ya
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani imekuja kwa lengo la
kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Makao
Makuu ya Trafiki, Dar es Salaam, ASP Abel Swai akitoa elimu ya usalama
barabarani kwa abiria, muda mfupi kabla ya kuanza safari za mikoani katika
kituo Kikuu cha mabasi Ubungo, jijini Dar es Salaam, elimu ambayo inalenga
kudhibiti ajali za barabarani kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka. (Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments: