By: Mohab Dominic
on 06:28
/
|
Kijana huyu anaitwa "Simon Shilage"
ana umri wa miaka 22, Yeye kwa kushirikiana na mwenzie mmoja ambaye bado
hajapatikana ndio waliomuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba
Ndg.Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.
Kijana huyu amekamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota
akijaribu kutoroka. Amekutwa na panga lenye damu alilotumia kumuua
diwani Muliga. Alipohojiwa amekiri kwamba ni kweli yeye na mwenzie mmoja
(hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe.Muliga kwa kumkata mapanga.
Amesema kazi hiyo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo
kwa ticket ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa
Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi. Ameongeza kuwa Mgombea
huyo aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua
Muliga na aliwapa "advance" ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=).
Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake
majira ya saa 2 usiku akiangalia "Taarifa ya Habari" ambapo walimkata
mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea
kusikojulikana. Kijana huyu alikamatwa na wananchi wenye
hasira kali ambao walitaka kumuua lakini akaokolewa na Polisi. Hata
hivyo wananchi hao walifanikiwa kumkata sikio lake moja la kushoto kama
anavyoonekana pichani. Kwa sasa anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.!
|
Tag:
matukio
MOHABMATUKIO.BLOGSPOT.COM's Admin
We are.., This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
No comments: