sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » IMF: UCHUMI WA TANZANIA WAONGEZEKA AFRIKA MASHARIKI

                                                                                       
 RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA JOHN MPOMBE MAGUFULI . 
 
  Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola. 

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016

Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika ripoti yake iliyotolewa nchini Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .

Image caption Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016. 

Ivory Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa asilimia 6%.

IMF hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.

Kwa mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.

  Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola. 

Mataifa yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile Nigeria na Angola.

Aidha Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba yake.

Ripoti hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.

Katika orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
1.    Ivory Coast 8.5%
2.    Tanzania 6.9%
3.    Senegal 6.6%
4.    Kenya 6%
5.    Zambia 3.4%
6.    Nigeria 2.3%
7.    Afrika Kusini 0.6%


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply