Wanajeshi hao wa Uingereza
watasaidia wanajeshi wa AU
Wanajeshi
wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na
wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.
Wanajeshi
hao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi
waliowasili Somalia ni 10 na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika
(Amisom) kukabiliana na al-Shabaab.
Idadi
ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 sana
wakihusika na shughuli za matibabu, mipango na uhandisi.
Wapiganaji
wa al-Shabaab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia kudhibiti maeneo ya
nchi hiyo.
Wamekuwa
wakitekeleza msururu wa mashambulio ndani ya nchi na pia nje ya nchi, hasa
katika nchi jirani ya Kenya.
Kundi
hilo linakadiriwa kuwa na wapiganaji kati ya 7,000 na 9,000.
Kikosi
cha Amisom kilizinduliwa mwaka 2007 na kina wanajeshi kutoka Uganda, Burundi,
Djibouti, Kenya na Ethiopia.
|
No comments: