sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » MAHAKIMU SHINYANGA WATOA KILIO CHAO KWA RC JUU YA UKAMILISHWAJI WA JENGO LA MAHAKAMA KUU



Na
Shinyanga
Febr 4, 2013.
 HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO WILAYANI KAHAMA MH BRYARUGABA AKIWA NA ASKARI  AFANDE THOMAS SIKU YA SHERI TANZANIA

BAADHI YA WANASHERI WAPONGEZANA KATIKA SIKU YA SHERI KATIKA  VIWANJA VYA MAHAKANI WILAYANI KAHAMA

 
MAHAKIMU SHINYANGA WATOA KILIO CHAO KWA RC JUU YA UKAMILISHWAJI WA JENGO LA MAHAKAMA KUU

UONGOZI wa Mahakama ya Mkoa wa Shinyanga umemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kuiomba Serikali kuharakisha ujenzi wa Mahakama Kuu  ya Mkoa wa huo ili Mkoa uweze kunufaika na huduma za Mahakama kuu badala ya kuendelea kufuata huduma hiyo Mkoani Tabora.

Ombi hilo lilitolewa jana  na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama Mkoa wa Shinyanga John Meseka katika Sherehe za maadhimisho ya siku ya Sheria Dunia zilizofanyika viwanja vya Mahakama ya Mkoa Mjini Shinyanga.

Meseka alisema kuwa pamoja na Changamoto ya ukosefu wa Mahakama kuu katika mkoa wa Shinyanga pia wanakabiliwa na uhaba pamoja na uchakavu wa miundombinu  hususani majengo ya Mahakama ingawa mpaka sasa bado yanatumika katika shughuli nzima za kimahakama.

Alisema jengo hilo la Mahakama kuu ambalo ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2008 lakini mpaka kufikia sasa bado jengo hilo halijakamilika  kwa matumizi ya shughuli za kimahakama kuu kutokana na sababu nyingi ikwemo ukosefu wa fedha.

“Kwa maneno mengine tunakuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga    uingilie kati katika suala hili  ili jengo letu liweze kukamilika  na Wananchi waanze sasa kunufaika kwa kupata huduma  ya Mahakama Kuu  katika Mkoa wetu wenyewe”Alisema Hakimu John Meseka Chaba.

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi Mfawidhi Seth Mkemwa akitoa salamu zake alisema moja ya Vikwazo vinavyosababisha ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama mbalimbali ni pamoja na ukiritimba uliopo wa kimahakama na kuongeza kuwa ni bora mshitakiwa akasomewa mashitaka na kesi yake ikasomwa siku hiyohiyo kama mashahidi watakuwepo wa kutosha.

Alisema kuwa Changamoto nyongine ni pamoja na mashahidi kuwa na woga wa kutoa ushahidi katika kesi mbalimbali huku wakijua kuwa Mahakama sio rafiki na watu wa kundi hilo hali ambayo inakuwa vigumua katika kuendesha kesi mapema.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mwanasheria kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Lightness Tarimo lisema kuwa uchelewashwaji wa mashauri kufika kwa muda katika mahakama mbalimbali ni moja ya matatizo yaliopo katika mkoa huu.

Alisema kuwa Mapango wa Matokeo makubwa  sasa ni bora ukatumika katika ukamilishwaji wa Jengo la Mahakama Kuu  ya Mkoa wa Shinyanga hali ambayo itapunguza mwendo mrefu wa kufuata huduma hiyo Mkoani Tabora na kuongeza kuwa kwa mwaka huu wangefurahi kama sherehe hizo zingefanyika katika jengo hilo.

Aidha alisema kuwa kwa sasa ataendelea kusisitiza juu ya ujenzi wa Jengo hilo la Mahakama kuu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mahakama za Mwanzo ambazo pia zenyewe zimeonekana  kuwa pungufu katika mkoa wa Shinyanga.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply