POLISI WANNE WAUWA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI KATIKA BANK YA CRDB MBANDE WILAYANI TEMEKEMasaa machache baada ya kutokea tukio la askari polisi kuuawa jijini Dar es salaam usiku wa Agosti 23,2016,   


Masaa machache baada ya kutokea tukio la askari polisi kuuawa jijini Dar es salaam usiku wa Agosti 23,2016,waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio.

Hii ndiyo taarifa Kutoka kwa Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba aliyoitoa usiku wa Agosti 23,2016 

"Usiku huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.
 
Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
 
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu"
POLISI WANNE WAUWA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI KATIKA BANK YA CRDB MBANDE WILAYANI TEMEKE POLISI WANNE WAUWA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI KATIKA BANK YA CRDB  MBANDE WILAYANI TEMEKE Reviewed by Mohab Dominic on 21:45 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.