sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » ADAKWA AKIMBA SANDAKA KANISANI

nduku cha sandaka ambapo wizi aliimba  sandaka 

hili ndiyo kanisa ambalo wauumi wake wakati wa kusali jemba moja likachota sandaka 

Wakati mchungaji na waumini  wa kanisa la EAGT (JERUSALEMU) lililopo kata ya majengo wilayani Kahama mkoani  Shinyanga wakiwa katika maombi mazito huku wakiwa wamefumba macho kama ulivyo utamaduni wa makanisa yanayojiita kuwa ya kiroho muumini mmoja alitumia fursa hiyo kuchota fedha za sadaka.

Tukio hilo la aina yake lililovuta hisia ya watu wengi limetokea jumapili april 9 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni wakati mchungaji Gwamiye akiongoza maombi kwa waumini wake huku wakiwa wamefumba macho ndipo muumini  mmoja alijifanya anatoa sadaka kasha kuchota shilingi 2,000 ndani nduku.

Mmoja wa waumini wa kanisa hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema licha ya muumini huyo kudokoa shilingi 2,000, siku hiyo hiyo misa ya asubuhi muumini huyo alidakwa na mashemasi wa kanisa hilo baada ya kuchukua fedha isiyofahamika wakati alipoungana na waumini wengine kwenda kutoa sadaka ambapo hata hivyo alisamehewa.

“Huyu jamaa anayejiita kuwa ni muumini wa kanisa hili siku hiyo hiyo ya jumapili majira ya asubuhi alisamehewa na mashemasi wa kanisa hili baada ya kuchukua kiasi cha fedha ambacho ambacho walisema ni kikubwa bila kufafanua huku wakidai pengine alikosa fedha ya kujikimu kimaisha,” alisema muumini huyo wa kanisa la EAGT Majengo bila kutaja jina.

Hata hivyo baadhi ya waumini walidai kushangazwa na kitendo hicho cha vibaka kuanza kuingia katika nyumba mbalimba mbali za ibada kwa lengo la kuiba sadaka bila kumwogopa mungu.

Naye mchungaji wa kanisa hilo Felix Gwamiye alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo kanisani kwake na kusema kuwa kwa sasa kuna wimbi la vibaka wanaoingia ndani ya makanisa wakati maombi yakiendelea huku wakati wakiwa katika maombi mazito wao ndipo wanapata mwanya wa kudokoa fedha za sadaka.

Katika tukio hilo Gwamiye alitoa wito kwa makanisa ya kipentekostal wilayani hapa kukaa chonjo na vibaka wanaoingia kanisani na kujifanya ni waumini kumbe wanavizia sadaka za waumini.

“Mtuhumiwa huyo alikamatwa na mashemasi wakati alipomuona akiiba hela za sadaka baada ya waumini kumaliza kutoa sadaka na kuanza maombi, mimi kama kiongozi wa kanisa hili nimemsamehe lakini asithubutu kuingia katika makanisa yoyote hapa Kahama  maana waumini wakiamua kufunga novena ya maombi laana itamsumbua,” alisema Gwamiye.

Hata hivyo katika mahojiano yake na gazeti hili muumini huyo aliyejitamburisha kwa jina la Dismas Simoni(35) mkazi wa Kata ya Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita alisema kuwa ni shetani ndiye aliye mtuma na kujikuta anadokoa kiasi hicho cha fedha na kumuahidi kiongozi huyo wa kanisa kuteua watu wa kuongozana nao kwa ndugu yake hali ambayo ilimfanya Gwamiye amsamehe.

“Mimi ni mkazi wa kata ya Ushirombo Bukombe huku Kahama nimekuja kumtembelea kaka yangu anayeishi kitongoji cha Nyamhela kata ya Mhongolo binafsi niseme nimepitiwa tu na shetani samahani sana kama mtanisamehe naweza kurudisha hela niliyochukua asubuhi nah ii 2,000/= siewezi kurudia kosa jamani,” alisema mtuhumiwa wa kuiba sadaka.

Mwisho.

  

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply