sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » AKUTWA NA MAGUNI 10 YA BANGI NYUMBANI KWAKE

 Mtuhumiwa wa  wizi wa kuvuja maduka na nyumba za watu Antony Boniphace (21)

 Baadhi ya mmagunia ya bagi kati ya kumi yalikamatwa nyumbani kwa Makongolo Mafundo (32) 

 Mkuu wa upelelezi wilaya ya kahama Georger Bagemu akionyesha baadhi ya maguni ya bagi kati ya kumi 

 Magunia ya Bagi ambayo yamekatwa na jeshi la polisi kahama 

 Magunia ya bagi yakiwa katika kituo cha polisi kahama 


KAHAMA 

JESHI la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linamshikilia Makongolo Mafundo (32) mkazi wa kijiji cha Sigili tarafa ya Itobo Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora kwa kosa la kukutwa na magunia 10 ya bagi yenye ujazo wa kilo 350.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ACP Murilo Jumanne Murilo amedhibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 12 mwaka huu akiwa nyumbani kwake baada ya kukutwa na magunia kumi ya bangi.

Kamanda Murilo alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo nyumbani kwake huko katika kijiji cha Sigili kilichopo mpakani mwa Isaka Wilaya  ya Kahama na Nzega Mkoani Tabora baada ya kukutwa na kidhibiti cha magunia hayo ya bangi.

Aidha Kamanda huyo alisema kuwa baada ya jeshi la Polisi mkoani  humo kumbana  mtuhumiwa huyo alitaja sehemu anakotoa bangi hizo  kuwa ni Mambali Nzega  mkoani Tabora na kutaja asilimia kubwa ya wateja wake wanatokea jijini Mwanza na bangi hizo zilikuwa tayari kwa kusafirishwa kwenda Mwanza.

Alisema katika Tukio hilo pia nyumbani kwa mwanamke mmoja mkazi wa maeneo hayo aliyefahamika kwa jina la Pili Kizota Polisi wamekuta Bangi magunia makubwa 4, na debe 4 zilizotelekezwa ndani huku mtuhumiwa akitokomea kusiko julikana.

Kamanda Murilo ameapa kuendeleza msako mkali dhidi ya watu wanaoendelea na biashara ya madawa ya kulevya katika Mkoa wake wa Shinyanga.

Wakati huo huo Murilo alisema kuwa watu watatu akiwamo na aliyejidai ni usalama wa Taifa wanashikiliwa na jeshi la Polisi wilayani Kahama kwa  uchunguzi wa makosa yao kisha watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply