sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » TUNZENI WATOTO MNAOZAA NJE YA NDOA; NKURLU

 Mkuu wa wa wilaya ya kahama Fadhiri Nkurlu siku ya kilele cha mtoto wa Afrikani ambapo kimkoa yalifanyanyka uwanja wa shule ya msingo mwendakulima 

 Mwenye suti ni Diwani wa kata ya mwendakulima pius Emmanuel, na mchumi wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya kahama  

 Mwenye shati ya darft ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa kahama Abel shija kwenye mahadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika 

Mwanafunzi 

Wanafunzi wakionyesha vifaa vyao ya utendaji kazi zao 

 Mwalimu wakiwa na watoto wao katika siku ya mtoto wa Afrika 

  Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza mgeni rasm mkuu wa wilaya ya kahama Fadhiri Nkurlu 

 Bango la siku ya mtoto wa Afrika 

 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kutimiza wajibu wao siku ya watoto wa Afrika kimkoa ulifanyika katika mji wa halmashauri ya mji wa kahama ambapo mahadhimisho yake yamefanyika katika kata ya mwendakulima 

 Baadhi ya wakuu  wa idarra  mbalimbali wa halmashauri ya mji wa kahama 

 Watendaji wa kata na mitaa katika sherehe ya siku ya mtoto wa Afrika 
KAHAMA 

MKUU wa Wilaya ya Mkoani Shinyanga Fadhil Nkulu amewataka Wanaume walizaa nje ya ndoa mjini hapa kuhakikisha kuwa wanawatunza watoto wao waliozaa nje ya ndoa, kama wavyowatunza waliozaa ndani ya ndoa katika familia zao.

Nkurlu aliyasema hayo juzi katika kilele cha siku ya mtoto wa Afrika ambayo kimkoa ilifanyika katika kta ya Mwendakulima katika Halmashauri ya mji wa Kahama na kuongeza kuwa kwa sasa ofisi yake itahakikisha kuwa inawatafuta watu hao.

Alisema kuwa wazazi wenye tabia kama hiyoya kuzaa nje na kuwatelekeza watoto wao wanatambulika katika ofisina kuongeza kuwa hali hiyo haiatavulimiwa  na watotoambao wanawatambua wazazi wao lazima warudishwe kwao.

“Haiwezekani kwa Mwanaume mzima uzae nje ya ndoa na kisha kuacha kumtunza wanao hali inachangia kwa kiwango kikubwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaishi katika mazingira maumu huku wazazi wao wakiwepo tuu”, Alisema Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu.

“Mnapo zaa nje ovyoovyo mnategemea nani awatunzie watoto wenu kwani mnapokuwa katika maeneo ya faragha kwani sisi huwa tunakuwepo? Nawaambieni nyinyi  mnaozaa nje ya ndoa sasa hivi ofsi yangu inawatafuta na tutawachulia hatua za kisheria kwa kutotunza watoto”, Alisema Nkurlu

Mkuu huyo wa Wilaya aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ZainabTelack aliyekuwa Mgeni rsmi katika Sherehe hizo, alisema Mkoa wa Shinyanga una jumla ya watoto 54, 352 wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuongeza kuwa hali hiyo inachangiwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na umasikini wa kipato na kuvunika kwa ndoa.

Nao watoto waliohudhuria maadhimisho hayo wakisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi, walisema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwapo ile ya kutokuwepo kwa maabara atika shule za Sekondari hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa Elimu katika Mkoa wa Sinyanga.

Akisoma Risala hiyo Ester Aloyce alisema kuwa changamoto nyingine ni kuitaka Serikali kutoa Elimu bila ya kuwa na malipo hadi katika kiwango cha sekondari ili kufanya kila Mwananchi wa hali chini kuweza kusomesha watoto wake.

Kwa uapnde wake Mwanafunzi kutoka katika shle ya Sinuka Christina Simea alieataka wazazi kujenga utamaduni wa  kufuatilia maendeleo ya watoto mashuleni ili kuona changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika masomo.

Aidha Simea alisema kuwa wapo wazazi ambao hata haakagumi madaftari ya watoto wao wanapokuwa wakitoka shule  kwa mwaka mzima ikiwa pamoja na pamoja na miihani ambayo ambayo wanafunzi wanakuwa wakiiifanya ya kujipima kila wakati.

Hatahivyo pamoja na mambo mengine Simea aliwataka Wazazi angalau kutenga hata siku moja atika juma kukaana familia zao ikiwa ni pamoja na watoto hali ambayo itasaidia katika kuleta pendo na amani katika  amilia husika.

“Sisi kama watoto tunaomba wazazi kutenga hata muda wa siku oja dani ya wiki ili kukaa na sisi na kuzungumza kuona changaoto ambzo zinakuwa zikitukabili watoto tunapokuwa nyumbani au shuleni na kuweza kuzifania kazi”, Alisema Smea Mwanafunzi wa kidato chatatu katika shule ya sekondari ya Sinuka.

Kilele cha Sherehe za siku ya mtoto wa Afrika  katika Mkoa wa Shinyanga zilifanyika katika kata Mwendakulima katika Halmashauri ya Mji wa Kahama huku kauli mbiu ikiwa Maendeleo endelevu 2030, imarisha ulinzi na fursa kwa watoto.«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply