sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » Rais Magufuli: Waliotuibia Madini Yetu Wengine ni Viongozi Wakubwa

 Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, John Magufuli anazindua mradi wilayani Sengerema. Anaeongea kwa sasa ni katibu mkuu wizara ya maji, Prof Kitila Mkumbo ambae anatambulisha wageni waliohudhuria na kutoa taarifa fupi ya mradi huo. Tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.




Kitila Mkumbo: Mradi unagharimu jumla ya bilioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imetoa bilioni 10.6 katika fedha hizo na ulianza 2011 na unatarajiwa kukamilika Disemba 2017.

William Ngeleja(MB-Sengerema): Mheshimiwa Rais, nimesimama kwa niaba ya wananchi na uongozi wa Sengerema, mwaka jana ulikuwa na sisi na ulizungumzia maendeleo pamoja na mambo mengine, leo mwaka haujaisha uko tena na sisi, tunakushukuru sana. Tuliopo hapa tuliteseka sana, tunashukuru sana.

Wana Sengerema tunaahidi kuilinda miundombinu hii ya maji, tunawatambua wadau bei ya maendeleo Afrika Ambao wametuwezesha kufika hapa, nakushukuru sana mheshimiwa Rais.

Charles Tizeba(MB-Buchosa): Mwenzangu ameshakukaribisha hapa Sengerema, watu wana hamu ya kukusikiliza wewe. Huenda huu ni mradi mkubwa umetekelezwa katika kanda hii hivi karibuni.

Ukamilifu wa huu mradi kwetu ni manufuu makubwa sana ikiwemo kwa wananchi wa Buchosa, wananchi wa huko wana hamu sana na wewe ukawatembelee, asante sana.

John Mongela(Mkuu wa Mkoa-MZA): Nisipoteze muda, nirudie shukrani kwa mapenzi yako kwetu, leo wote ni mashahidi pamoja na miradi mingi iliyotolewa taarifa, Magu kuna mradi mkubwa, Misungwi mkandarasi anapatikana, tunakushukuru sana na mkoa wetu ni shwari.

Kama itakupendeza, tayari tuna viwanda 12 vipo tayari kwa ufunguzi, inaonyesha utekelezaji ni mkubwa sana na wenye wasiwasi waje kushuhudia.

Mwaka huu tunategemea kuvuna si chini ya kilo milioni 20 za pamba, kwa ridhaa yako mengi yanafanyika kwenye nchini, tungeomba katibu wa CCM, karibu sana.

Katibu CCM Mkoa: Ratiba hii ya kwako lakini tunaomba upate ushuhuda mdogo, kwa kazi unayofanya wanachama 900 wameamua kuja chama cha mapinduzi. Namleta shuhuda mmoja ambaye anaitwa Tabasam, kavaa gwanda, sisi tutamvisha kofia ya CCM.

Tabasam: Mheshimiwa mgeni Rasmi, nakuomba radhi sana, ni kweli nimeruka na chopa nikikupiga vita, kwanza naomba unisamehe sana. Tumezungumza sana kupitia CHADEMA kwa kupotosha, sio mimi peke yangu niliyejitoa ufaham, wapo wengine ndani ya chama cha mapinduzi waliojitoa ufahamu.

Mto uliopita sakata la madini una maji ya moto, tutavuka na wewe. Kwa mikataba hii unayoiandaa, wapo wametoka Canada wapo tayari kwa mazungumza. Kuna watu wa aina nne unatakiwa kuwachunga sana

1.  Wanasiasa katika vyama vya upinzani na wanafiki ndani ya chama cha mapinduzi
2.  Wafanyabiashara na wanasiasa wasiotaka kulipa kodi
3.  Wapiga dili wanaokaa vijiweni na kwenye kahawa tangu asubuhi
4.  Watumishi wa serikali ambao wanasema wewe bado wewe ni waziri wa ujenzi

Magufuli Oyee, anakaba mpaka penati. Naomba mheshimiwa Magufuli nikupe kabisa kadi ya CHADEMA iliyolipiwa mpaka 2020, kuna watu leo hatalala kwa Tabasam kuonekana mubashara kwenye TV.

Mwakilishi, Bonde la ufa: Napenda kutoa shukrani nyingi, asante kwa kutualika. Hii ni moja wapo katika ushirikiano wa Afrika Mashariki, nashukuru ushirikiano wa Tanzania katika mradi huu ikiwemo kuchangia asilimia 15, mradi huu ambao thamani yake ni zaidi ya dola milioni 125 kwa nchi zote za Afrika Mashariki na jumla ya watu zaidi milioni 2 watanufaika.
=======

Kwa sasa Rais Magufuli anasikiliza malalamiko ya mama ambaye analalamika kubobolewa nyumba na DC kupitisha barabara baada ya kulalamika kuhusu tatizo la umeme na jirani yake tajiri kuzuia, Rais ameagiza mkuu wa Mkoa kwenda kwenye plot ya mama husika(Rosemary Simon) haki itatendeka na atapelekwa taarifa, pia ameagiza vyombo vya dola kumlinda.
=========

Magufuli: Wana Sengerema, maji yamekuja, katika wilaya zilizokuwa na matatizo ya maji ni pamoja na Senngerema. Nimeishi Sengerema na ninaijua yote, nimekuwa mwalimu wa hapa Sengerema. Shida ilikuwa ni kubwa, ulikuwa unapata maji asilimia 33.

Nafurahi kuona mradi huu ulifanikiwa, lita karibu 20,000 zitakuwa zinapatikana za maji, mradi huu ni muhimu, utanufaisha pia vijiji vya jirani.

Kufanya uvuvi kwa kutumia madawa, yataingia ziwani na kuvutwa. Utawapa watu maji na kemikali, utaleta madhara kwa watanzania wengi, kansa, kuharibika mimba, wanaume nao nguvu zinaharibika, wanawake nguvu zinaharibika. Ninazungumza nguvu za kulima, ndugu zangu mnatafasiri mno.

Tunataka watanzania wote wapate elimu bure, kwa watoto walio kando ya ziwa ni kwenda kuvua samaki wakikosa ada. Tumeamua karo zote mpaka sekondari zitalipwa na serikali. Ninachowaomba wazazi na watoto, wakasome kwelikweli.

Kumekuwa na watu wanazungumza hata waliopata mimba wakasome, nikusomeshe bure na wewe ukapate mimba bure, haiwezekani, kafate kilichokupeleka kusoma.

Tukiruhusu jambo hili tutakuwa tumeingia kwenye mtego wa ajabu, akishapata mimba, mchezo ameshauzoea na yeye atakuwa mwalimu wa wanafunzi wengine.

Tuache mambo ya kukopi, nimekaa Ulaya, kwao wanafunzi hawapati mimba. Sio kwamba nawachukia waliopata mimba, wakatafute shule nyingine zisizo kwenye mfumo wa serikali. Nawaomba NGO wawafungulie shule zao, wataenda kusoma, nimeshasema hakuna, waimbe, wazunguke, mimi ndiye Rais.

Ni ukweli pia hatujawahi kurudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba, kumekuwepo ujanja kwa walimu, mwalimu mkuu atakaerudisha shuleni mwanafunzi aliezaa anaondoka.

Juzi mliona kwenye TV wanafunzi wanafanya umalaya, wakipata mimba na wenye wamebakwa?

Mlinichagua kwa kuwaeleza ukweli, lazima niwaeleze ukweli.

Tumekuwa na miradi ya hovyo kwenye umeme, sitaki kuzungumzia kwa sababu mengine bado kesi iko mahakamani. Tunapokuwa na viwanda vya kutosha, watanzania wengi watapata ajira.

Waliovichapa viwanda wapo, wameshusha hata wakulima kukata tamaa ya kulima. Watanzania wapate ajira na wapate fedha, Kiwanda cha Nyakarilo kinafanya kazi? Kulikuwa na mafuta, havifanyi kazi.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply