sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » WATU WATATU WACHOMWA MOTO MJINI KAHAMA NA NYUMBA MOJA KUTEKETEZWA,WAKITUHUMIWA KUHUSIKA NA UPORAJI WA BODA BODA



Mkuu wa polisi wilaya ya kahama OCD  Mussa  Mchenya akiangalia mili ya watu wawili waliouwa kwa kuchomwa na moto katika mtaa wa kitwana 


 


 
MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA KITWANA AKIWA ENEO LA TUKIO AMBALO WATU HAO WAMECHOMEWA.

NYUMBA YA MMOJA WA WATUHUMIWA IKIENDELEA KUWAKA MOTO,KATIKATI NI PIKIPIKI ILIYOKUTWA KWENYE SHIMO LA CHOO IKICHOMWA.

BAADHI YA MADERAVA BODA BODA NA WANANCHI WAKIWA KATIKA ENEO LA MAKAZI YA MMOJA WA WATUHUMIWA WAKISHUHUDIA NYUMBA IKITEKETEA.

OCD WA WILAYA YA KAHAMA MUSSA MCHENYA MWENYE KOFIA NYEUSI AKIWA ENEO LA TUKIO AKISHUDIA ENEO AMBALO WATUHUMIWA HAO WAMECHOMEWA MOTO.

WANANCHI WAKIWA KATIKA MAKAZI YA MTUHUMIWA ALIYECHOMWA MOTO WAKISHUDIA NYUMBA IKITEKETEA.

NYUMBA IKIENDELEA KUTEKETEA ENEO LA SOFIA KAHAMA.
 
 

AFISA WA JESHI LA POLISI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ERICK AKIENDESHA PIKIPIKI YA MMOJA WA DEREVA BODA BODA AMBAYO ALIKUTWA ENEO LA TUKIO NA KUKAMATWA KWA LENGO LA KUSAIDIA POLISI.

MAAFISA WA POLISI WAKIWA KATIKA ENEO AMBALO TUKIO LIMETOKEA KATIKA PORI LA KITWANA KARIBU NA SHULE YA MSINGI.

SHIMO AMBALO MTUHUMIWA INADAIWA ALIFICHA  PIKIPIKI TATU NDANI YAKE.

WANANCHI WAKIENDELEA KUBOMOA NYUMBA YA MTUHUMIWA

ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO BAADA YA KUCHUKUA MIILI YA WATUHUMIWA WALIOCHOMWA MOTO.


MAAFISA WA POLISI WAKIWA WAMEIFIKISHA MIILI YA WATUHUMIWA  KWENYE CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA.


KAHAMA

Wananchi waliojichukulia Sheria mkononi leo wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama, kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.
  
Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea wizi wa Pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa leo majira ya saa nne asubuhi.

Wakizunguz Mashuhuda katika tukio hilo  wamesema mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa  aliwataja wenzake wawili waliouawa leo baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana ,peter joseph   amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao imechukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama,

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply