Na Mohab
Dominick
Kahama
Oct 28 2013.
MAMLAKA ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA)
imetakiwa kuangalia upya sheria ua jengwaji wa vituo vya mafuta katika maeneo
mbalimbali hususani Wilayani Kahama ambapo vituo hivyo vimekuwa vikijengwa ovyo hadi katika maeneo ya makazi ya watu.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama
Ernest Masanja kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya katika kikao
cha taftishi ya kujadili ombi la kurekebisha bei za huduma za Mamlaka ya maji
safi na usafi wa mazingira (KUWASA).
Masanja alisema kuwa kwa sasa kumekuwa na mrundikano
wa vituo vya mafuta ambavyo vimekuwa vikijengwa ovyo hadi katika makazi ya watu
hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa
inapotokea ajali.
Alisema kuwa katika Mji wa Kahama kwa sasa vituo
hivyo vimejengwa hadi katika makazi ya watu na kuwataka viongozi wa Mamlaka
hiyo ya kudhibiti wa Nishati na maji kuangalia sheria upya inasemaje ili kuweza
kudhibiti ujenzi huo ambao umekuwa kero katika Wilaya .
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa EWURA
George Kaberwa alisema kuwa suala amelichukua na kuhaidi kuwa atalifikisha
katika ngazi husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi na majibu yatatolewa muda
utakapowadia.
Nae Meneja wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira Wilayani Kahama (KUWASA) Joel Rugemarila akizungumzia kuhusu angezelo
la Bei ya Maji katika Mkutano huo ambo ulijumuisha wadau wa maji alisema kuwa
ametoa mapendekezo ya kuongeza bei za kutoka shilingi 595 hadi 970 kwa matumizi
ya myumbani.
Rugemarila alisema kuwa kwa kuongeza bei hizo za
maji kutasaidia kwa mamlaka yake kuweza kuwa na uhakika wa kununua maji kutoka
kwa wauzaji wake ambao ni Mamlaka ya maji safi na maji taka Kahama na Shinyanga
(KASHWASA).
Pia kutasaidia katika kuwa na uhakika wa maji masaa
24 na kuhakikisha kuwa mtandao wa maji unawafikia walaji wake kwa muda muafaka
na watu wengi hasa katika maeneo ya mbali ambayo watu wanaishi.
Katika kikao hicho ambacho hata hivyo hivyo wadau
hao wa maji ambao kwa asilimia 51 ni wakazi wa majumbani wakalikataa
mapendekezo hayo kupandisha bei ya maji na kuitaka mamlaka hiyo kuangalia
vyanzo vyake vya fedha na kuongezea na sii kumchangisha mlaji ambaye sii kazi
yake.
mwisho
No comments: