Na Mohab Dominick
Kahama
0cto 28,2013.
KATIKA kuhakikisha Wanafunzi wa kike wanapata elimu sawa na
wale wa kiume hali imekuwa kinyume katika shule ya sekondari ya Mweri Wilayani
hapa ambapo jumla ya wanafunzi wa kike 48 walioanza kidato cha kwanza kwa mwaka
huu katika shule hiyo lakini mpaka kufikia hivi sasa ni wanafunzi wa wawili tuu
wa kike wanatarajia kufanya mtiahani wa kidato cha nne.
Hayo yalisemwa juzi wanafunzi wa Shule hiyo katika Risala
yao mbele ya Mdau mkubwa wa Elimu
Wilayani Kahama Eliasi Ku
Katika Risala yao hiyo Wanafunzi hao pia waliwaomba wazazi
kuwa na utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya Wanafunzi katika shule hali ambyo
inaweza kuchangia mahudhuri ya wanafunzi kuongezeka hasa kwa wanafunzi wa kike
ambao ndio imekuwa tatizo kubwa shuleni hapo.
Walisema kuwa katika shule hiyo jumla ya Wanafunzi 70 waliopo
katika shule hiyo wa kidato cha nne walianza kidato cha kwanza kwa mwaka huu
huku wsasichana wakiwa 22 lakini hadi kufikia hivi sasa ni Wanafunzi wa kiume
20 na wa kike wawili ndio wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha
nne kwa mwaka huu.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika mahafali hayo Elias
Kuandikwa alisema kuwa kama mzazi atatimiza wajibu wake katika jamii basi hakuna mtoto wa kike
atakayekosa Elimu kwa ajili ya mzazi
kutokuwa na karo au sare ya nguo za shule.
Kuandikwa aliwataka wazazi na Walezi katika kata hiyo ya
Ushetu kuhakikisha kuwa wanafuatilia maendeleo ya Wanafunzi wao hasa wale wa
kike na kuongeza kuwa ni jambo la ajabu kwa wazazi kuwa na visingizio vingi
wakati kumsomesha mwanafunzi ni jukumu lao la msingi.
Kuandikwa aliendelea kutoa masikitiko yake kuwa ni aibu wazazi wenzangu kijiji kizima na kata
yaUshetu kwa ujmla kuona ni wanafunzi wawili tu ndio wanatarajia
kumaliza kidato cha nne kwa mwaka huu na
kuongeza kuwa hii ni fedhea kwa jamii nzima ya hapa.
Akisisitiza juu ya Suala la Elimu kwa sasa hapa nchni
Kuandikwa alisema kuwa Elimu kwa jamii kwa sasa kuna wajibu mkubwa wa pamoja kati ya watendaji wa serikali ya
kijiji na wananchi kujua wajibu wao kila moja ili tuwakomboe watoto wa kike
katika taifa hili.
“Hakuna kitu kizuri kama kuwa na moyo
wa umoja katika kuleta maendeleo na ni ngumu sana kama hatutakuwa na umoja
katika utendaji na kushilikiana na serikali katika suala zima la Elimu na
kuwakomboa watoto wetu hasa wa kike waliopo katika majarubu mengi wawapo
mashuleni”, anasisitiza Kuandikwa.
Mwisho.
No comments: