Ule usemi kwamba ukitaka elimu huna budi
kuitafuta "popote na kwa gharama yoyote" umewaingia wanafunzi wa
shule ya Msingi Mwampunga Bule iliyopo kata ya Mishepo wilaya ya Shinyanga
vijijini waliolazimika kubadilishana vyuma chakavu na wafanyabiashara wa bidhaa
hizo ili kupata mahitaji yao ya shule.
Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wazazi kukosa mwamko wa elimu hivyo kuacha kuwahudumia watoto wao mahitaji yao ya shule ambapo biashara hiyo inawasaidia wanafunzi hao kupata mahitaji muhimu kama vile madaftari, kalamu pamoja na mabegi ya kubebea madaftari.
Njia hii imebuniwa na baadhi ya wanafunzi wanaopenda elimu, jambo ambalo pia limeungwa mkono na walimu wa shule hiyo baada ya kuona ni mkombozi kwa wanafunzi hao.

Hii ni shule
ya Msingi Majahida iliyopo nje kidogo ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu ambapo
nusu ya wanafunzi wake hukalia mawe madarasani kutokana na uhaba mkubwa wa
madawati shuleni hapo.
Wilaya ya Bariadi inaongoza nchini kwa kuzalisha pamba asilimia 60, pia ina rasilimali ya madini pamoja na mifugo ya aina mbalimbali. mohab Dominick

No comments: