headlines

    9:53 PM

sponsor

sponsor

Slider

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » SERIKALI IMEOMBWA KUKAMATA WAFUGAJI NA SII KUANGAMIZA MIFUGO
 Mohab Dominic




KATIBU WA WAFUNGAJI NCHINI GEORGE KIFUKO AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI HAWAPO PICHANI PICHA ZA BAADHI YA WANACHINI WALIOFANYIWA UNYAMA NA ASKARI POLI MJINI KAHAMA JANA


Na
Kahama
Jan 27, 2014.

SERIKALI imeombwa  pindi inapokamata mifugo ya Wafugaji hususani Ng’ombe katika operesheni zake isichukue jukumu la kuiuwa mifugo hiyo bali wakamatwe wafugaji na kufikishwa katika vyombo husika vya  sheria kujibu tuhuma.

Hayo yalisemwa juzi na Katibu wa Chama cha Wafugaji Nchini (CCWT) George Kifuko wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini kahama juu ya epesheni zilizofanywa na Serikali za kuwaomndoa wafugaji katika maeneo ya Hifadhi.

Kifuko alisema kuwa kwa sasa Wafugaji wamekuwa na maeneo madogo kwa ajili ya malisho ya Mifugo huku sehemu kubwa za malisho zilichukuliwa na hifadhi za wanayama pori hali ambayo inachangia kwa kiasi fualani kwao kuingia katika maeneo hayo.

Alisema kuwa ni bora kwa sasa Serikali isiwape wawekezaji maeneo pia iangalie upande wa pili ili na wao pia wawe na maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo yao ambayo kwa kiasi kikubwa inazidi kuongezeka hasa katika jamii ya wafugaji.

Alisema kuwa kutokana na operesheni iliyofanyika hivi karibuni imewaacha wafugaji wakiwa masikini kwa baadhi ya Ng’ombe zilikamtwa na kuongeza kuwa kuna idadi ya Ng’ombe zaidi ya 4,000 wamekamatwa katika eneo la Bukundi.

Aidha Katibu huyo wa chama cha Wafugaji nchini aliendelea kusema kuwa jumla ya Ng’ombe 1,089 wamepigwa Risasi huku wengine wakifa kwa njaa sambamba na kukatwakatwa mapanga na kutoswa majini huku mbuzi na Kondoo wakiwa 315.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa kwa upande wa mifugo iliyopotea alisema kuwa, jumla ya Ng’ombe waliopotea katika operesheni hiyo wanafika 335 wakati nyumba 5,701 zikihofiwa kuchomwa moto na kuteketea.

Katibu aliiomba Serikali kulifutilia kwa ukaribu suala hili watu walihusika waweze kuwajibishwa na kuongeza kuwa kwa watu walioptelewa na mifugi ni bora wakafidiwa kwani wanyama hao hawana makosa katika opereheni hiyo.

Mwisho.

«
Next
.SLAA NA MNYIKA WAZIDI KUIBOMOA KAMBI YA ZITO. .CHOPA DR SLAA YA POTEA NJIA KATA YA UBAGWE KAHAMA
»
Previous
NSSF WATOA MSAADA WA VITANDA VYA THAMANI YA MILIONI KUMI 10 WIGEHE SEKONDARY SCHOOL
Pages 22123456 »

No comments:

Leave a Reply