sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» »Unlabelled » WATAKIWA KUTOCHAGUA DIWANI MBINAFSI NA MPENDA RUSHWA   

Na 
Kahama
Febr 4, 2014.

 KAMISHINA WA ADC MKOA WA SHINYANGA JUSTINE KIMISHA AKIHUTUBIA WANANCHI KATIKA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA UBAGWE WILAYANI KAHAMA BAADA YA DIWANI WA KATA HIYO KUFARIKI DUNIA MWAKA JANA JUSTINE ALIKUWA MGENI MHALIKWA KWA TIKETI YA TADEA
 JUSTINE KIMISHA MGENI MHALIKWA KWA TIKETI YA TADEA AKIHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA KATA YA UBAGWE KUHUSU RUSHWA
 MGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA (TADEA )MAJINJA LUBIZA AKIHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA  KATIKA KIJIJI CHA MAZILAYO KATA YA UBAGWE
 KAMISHI WA ADC JUSTINE KIMISHA AKISISITIZA KUNUNULIWA KWA SHAHADA ZA WAPINGA KURA NI KUKOSA HAKI YAKO YA KATIBA
 BAADHI YA VIONGOZI WAALIKWA KATIKA SIKU YA UZINDUZI WA KAMPENI YA UCHANGUZI WA UDIWANI WA KATA YA UBAGWE WILAYANI KAHAMA AMBAO HUNATALAJIWA KUFANYIKA SIKU YA TAREHE 9 ,2,2014 SIKU YA JUMAPILI
 PIA BAADHI YA VIKUNDI VYA NGOMA  BALI MBALI ZIKUWEPO KATIKA UZINDUZI HUO MWANA KWELA NA BAADHI YA WASANI
 MH DIWANI MTARAJIWA AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA ADC KATIKA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KIJIJ CHA MAZILAYO KATA YA UBAGWE
 BAADHI YA VIONGOZI WA TADEA WILAYA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA WAKIWA KATIKA MKUTANO WA UZIDUNZI WA KAMPENI YA CHAMA HICHO JANA
 BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA MAZILAYO KATA YA UBAGWE WAKISIKILIZA SERA ZA CHAMA CHA TADEA
WATAKIWA KUTOCHAGUA DIWANI MBINAFSI NA MPENDA RUSHWA

WANANCHI wa Kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameaswa kutokuchagua Diwani ambaye ni mbinafsi na Mpenda Rushwa katika harakati za uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika kata hiyo kutokana na aliyekuwa Diwani wake  kufariki Dunia mwaka jana.

Hayo yalibainishwa juzi na Katibu wa Chama cha TADEA Zakayo Kassana wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi huo katika kijiji cha Mazirayo Kata ya Ubagwe Wilayani Kahama ambapo kwa mwaka huu chama hicho kimeamua kumsimamisha Majinja Lubinza kugombea kiti hicho.

Kassana alisema kuwa kama Wananchi watamuweka Diwani ambaye atajali sana Maslahi yake na Rushwa kwa ujumla basi watakuwa wamejimaliza wenyeye kwani viongozi kama hao kwa sasa hawatakiwi kabisa katika jamii.

Aliwataka wananchi wa kata hiyo kuchagua kiongozi mpenda maendeleo ambaye atafanya kazi kwa maslahi ya Wanachi na sii chama anacotokea hali ambayo italeta chachu kubwa katika kuhamisisha m aendeleo katika sehemu husika.

“kwa nini tusiwape kipaumbel viongozi wanaopenda maendeleo?na chagueni mtu anayeweza kuwatumikia na sii kuchagua mtu anayetokana na chama fualani inaweza kuja kuwagarimu hapo siku za baadaye”Alisema katibu huyo wa chama cha TADEA.

Pia alitoa angalizo kwa wananchi kutokuuza shahada zao kwani kufanya hivyo wanapoteza haki yao ya kupiga kura na kusisiza kila mtu anapaswa kutunza shahada yake ili aweza kupiga kura kuchagua kiongozi wake.

Katibu huyo aliendelea kusisiza kuwa kwa kuchagua kiongozi anayeweza kutekeleza na  kusimamia misingi ya utawala bora pamoja na kutekeleza yale anayoagizwa na Wananchi wake huyo ndio atakuwa kiongozi bora katika jamii inayomzunguka na kuwataka kufanya maamuzi yalio sahihi.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama cha TADEA Majija Libinza akiongea wananchi wa Kijiji hicho alisema kuwa katika kipindi kichobaki ni kidogo cha uongozi na kusema kuwa kama atapata ridhaa ya kuwaongoza wananchi hao atajitahidi katika kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo cha tumbaku ambacho ni maarufu katika eneo hilo.

Uchaguzi katika kata ya Ubagwe unatarajiwa kufanyika hivi karibuni kutokana na aliyekuwa kiongozi katika kata hiyo Robert Mndula kufariki Dunia mwaka jana hali ambayo imefanya uchaguzi katika kata hiyo urudiwe huku vyama vitatu  vya CCM, Chadema pamoja na TADEA vikionekana kuchuana vikali kupata kiticho.

mwisho

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply