Na Mohab Dominick
Jun,11.2014
Kahama
MTU mmoja amekufa dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya
kufukiwa na Kifusi katika Shimo walilokuwa wakichimba Dhahabu kwenye Machimbo
ya dhahabu yaliyopo katika Kijji cha Ilindi kata ya Zongomera Wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Wachimbaji wadogo Mkoani Shinyanga, Nicodemas Majaba
alisema tukio hilo limetokea jana asubuhi majira ya saa nne ambapo Marehemu
huyo alikuwa akichimba dhahabu na wenzake mara ghafla wakashukiwa na
kifusi kilichosababisha kutokea kwa mauaji hayo.
Majaba alimtaja aliyepoteza maisha katika tukio hilo ni Ezekieli
Moshi (35) Mkazi wa kijiji cha Mhunze Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu na
wengine wawili waliojeruhiwa ni Jacob Omoro(35) mkazi wa katoro pamoja na
Njile Sospiter (30) mkazi wa bariadi.
Aidha katika hatua nyingine Majaba alisema kuwa
mashimo hayo yaliyoleta maafa yalikuwa yamesimamishwa kufanya kazi mpaka
hapo baaye yatakapotafutiwa ufumbuzi.
Hata hivyo pamoja na majeruhi hao kulazwa Katika Hospitali
ya Wilaya ya Kahama Mkoani shinyanga Mganga Mfawidhi Joseph Fwoma alisema kuwa
hajapata taarifa juu ya Majeruhi hao kulazwa katika hospitali hiyo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kihenya
kihenya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wachimbaji
wachukue tahadhari na kuacha kuchimba dhahabu katika mashimo yasiyokuwa rasmi.
mwisho
No comments: