Mc mwl tandise wa shughuli ya sherehe ya uzinduzi na harambee ya chama cha ushirika cha wajasiliamali wa bulyanhulu
Mgeni rasmini mkuu wa wilaya kahama benson mpesya mwenye kipasauti akitoa neno kwa wageni walikwa
Mwenye miwani ni mwenyekiti wa becos makoba akiteta jambo na mkurungezi wa halmashauri ya msalala patrick charles kwenye harambee ya wajasiliamali wadogo wadogo
Mkuu wa wilaya ya kahama benson mpesya akitoa jambo
Moja wa kinamama wa kikundi cha wajasiliamali wakitoa mchango wake wakati wa harambee hiyo
Baadhi ya viongozi wa becos wakiwa na mkuk wa wilaya ya kahama mwenye tai na mkurungezi wa halmashauri ya msalala wakati wa harambee
Baadhi ya wageni walikwa
Mwenyekiti wa becos makoba akitoa neno la shukurani kwa wageni walikwa
katibu wa becos akishukuru kwa michango yao
Mkuu karibu sana hayo ni maneno ya mc kwa kwa mkuu wa wilaya ya kahama mwenye tai nyeupe
Na Mohab
Dominick
Kahama
Julay 29, 2014.
WANANCHI pamoja na Wafanyabiashara wenye uwezo wa
kifedha waametakiwa kujitoa katika kuwasaidia wananchi Wajasiliamali wadogo
ambao hawana uwezo wa kuwa na mitaji mikubwa ya kufanya Biashara ili kuwainua
kiuchumi na kuweza kumudu maisha.
Katibu wa Chama cha Wajasiliamali wadogo kutoka
katika kata ya Bulyanhulu (BECOS) Mwita Bhoke aliyasema hayo juzi wakati
akiongea na blog hii muda mfupi baada ya kufanya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili kutunisha mfuko wa chama hicho.
Bhoke alisema kuwa lengo la kuchangia harambee hiyo
ni kutunisha mfuko wa chama hicho kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuweza
kuanzisha ushirika ambao ungeweza kuwasaidia wajasiliamali wadogo katika kata
ya Bulyanhulu.
Alisema kuwa chama hicho kinakabiliwa na changamoto
kubwa ya kutokuwa na mitaji pamoja na
masoko ya bidhaa na huduma katika
jitihada za kujikwamua katika umasikini
uliopo kwa wajasiliamali hao.
Katibu huyo aliendelea kusema kuwa chama hicho
kilianzishwa mwaka 2014 na kuongeza kuwa
wamepata wakati mgumu kwa kufanya
shughuli za ujasiliamali kutokana na
kutokuwa na mitaji ya kutosha pamoja na mafunzo na zana bora pamoja na
masoko.
Pia aliendelea kusema kuwa nje ya umoja huo pia
wamekosa fursa nyingi za kiuchumi kwa sababu ya kutoaminiwa kwa mtu mmoja mmoja na wadau wa kiuchumi akitolea mfano wa
Serikali pamoja na taasisi mbalimbali za maendeleo wamekuwa wakihamasisha
wananchi kujiunga katika vikundi ili
wapewe mafunzo.
Katibu huyo alisema kuwa katika kataya Bulyanhulu
kihistoria kuna shughuli za uchimbaji mdogomdogo unaoendelea tangu miaka ya 1990 huku ongezeko kubwa la
watu likikadiriwa kuwa ni jumla ya watu 50,000 kwa Vijiji sita hali ambayo
wakipata angalau mitaji ya kufanya biashara ndogo ndogo watakuwa wamejikomboa
kiuchumi.
Katika harambee hiyo iliyokuwa na lengo la kuchangia
kiasi cha shilingi milioni 20 lakini jumla ya shilingi milioni 16
zilichangishwa huku ikiwa ni pamoja na
ahadi mbalimbali kutoka kwa wafadhili pamoja na makampuni mbalimbali yaliopo
mjini Kahama.
mwisho
No comments: