Mkuu wa wilaya ya kahama Benson Mpesya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kungawa viwanja vya uchimbaji mdogo wilayani kahama .
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime wilayani kahama
Mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiongea na waadishi wa habari juu ya makapuni makubwa ya uchimbaji yalivyotoa maeneo yao kwa ajili ya wachimbaji wandogo.
Afisa madini wa wilaya kahama sophia mwenye miwa kati akiwa kati ya wajumbe wa kamati hiyo
Mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo pia ni mkuu wa wilaya ya kahama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani .
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime wilayani kahama .
Mkurungezi wa Halimashauri ya msalala patrick charles akiwa moja wa wajumbe wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya wachimbaji wadogo katika machimbo ya nyangalata na mwime .
Na Mohab
Dominick
Kahama
Agust 1, 2014.
HATIMAYE
Serikali kupitia Wizara ya Madini na Nishati imeanza kusikiliza kilio
cha Wachimbaji wadogowadogo kuhusu maeneo ya uchimbaji baada ya kuinyanganya
Kampuni ya African Barrick Gold na
Pangea Mineral baadhi ya maeneo waliokuwa yanaleseni za Kampuni hizo na hawayatumii
kisha kuwamilikisha wachimbaji wadogowadogo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyasema
hayo juzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu nia ya Serikali
kuanza kutatua matatizo ya Wachimbaji wadowadogo kuhusu maeneo yalikuwa na
leseni za wachimbaji wakubwa na kutoyafanyia shughuli za uchimbaji.
Mpesya alisema kuwa baadhi ya maeneo waliopewa
wachimbaji wadogo ni pamoja na eneo la Nyangalata ambaolo lilikuwa na leseni
Kampuni ya African Barrick Gold na eneo la Mwime ambalo lilikuwa likimilikiwa
na Kampuni ya Pangea Mineral.
Mkuu huyo wa Wilaya akiwa na Kamati ya watu saba ya
ugawaji wa Viwanja vya madini alisema kuwa Serikali ilitangaza kuwa itatoa
nafasi kwa wachimbaji wadogowadogo ambao kwa kaisi kikubwa wamekuwa wakivamia
na kuongeza kuwa katika maeneo ya Nyangalata na Mwime leseni ya Barrick imefutwa na kupewa
wachimbaji wadogowadogo.
Aidha aliendelea kusema kuwa maeneo hayo kwa sasa
hayana leseni na kuongeza kuwa ugawaji wa maeneo hayo utaangaliwa upya na
kuongeza kuwa kwa watu wanaotaka maeneo kwa sasa hawanabudi kuomba upya leseni
za kumiliki na hiyo ni kwa mujibu wa kamati ya ugawaji wa viwanja vya madini
ilivyopanga.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa maombi ya
kuomba yataanza kupokelewa kuanzia tarehe 2/8/2014 hadi kufikia tarehe
31/8/2014 na kuongeza kuwa anayetaka maeneo hayo nafasi ipo wazi lakini kwa
sasa maeneo hayo ni mali ya wachimbaji wadogowadogo wa maeneo hayo.
Pia aliwataka wachimbaji wadowadogo kuhakikisha kuwa
wanaunda ushirika na kuusajili na kungeza kuwa serikali inataka kuona
rasilimali hiyo ya dhahabu inanufaisha watanzanzania kuanzia katika ngazi ya
vijiji na Taifa kwa ujumla na kuhakikisha kuwa Wilaya ya Kahama inapata mgodi
wa tatu utakaotokana na wavchimbaji hao wadogo.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa Madini Kanda
Hamphrey Mmbando alisema kuwa kutokana na Serikali kuwakumbuka wachimbaji
wadogo ni suala la msingi kwani hapo awali walikuwa wakihangaika kuvamia maeneo
yenye leseni za Wachimbaji wakubwa au watafiti.
Alisema kuwa katika eneo la Mwabomba bado mazungumzo
yanaendelea vizuri baina mtafiti amayefanya kazi hapo ambaye ni Kampuni ya Rift
Valley Resouses na Kamati hiyo na kuongeza kuwa kama kutakuwa na makubaliano
mazuri basin a eneo hilo wanaweza kupewa wachimbaji hao wadogo.
Mwisho.
No comments: