Watoto sita, wakiwemo wawili wa
kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri
baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa
ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti na
wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la Feed Force, Kwamorombo
jijini Arusha.
Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa
la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa
mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi
2,000 za kufungia mdomo.
“Siku moja nilipofika shuleni
wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona
wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname
akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.
Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa
akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza
katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.
“Tukifika huwa wanatufungia ndani na
kutuambia tuwanyonye, baadaye wanatubaka na wakimaliza wanatuambia
tukisema kwa mtu yeyote watatuchinja na kutuzika ndani ya kanisa lao,” alisema denti huyo.
Wanafunzi hao walieleza kuwa
watumishi hao huwarubuni kwa kuwaeleza kuwa watawasaidia kuwasomesha iwapo
watakuwa wakienda kwenye kanisa hilo na kuwaingilia.
Mzazi mmoja wa watoto hao, Julius,
mkazi wa Kwamorombo alisema mtoto wake alimweleza kwamba amekuwa akifanyiwa
mchezo mbaya na watumishi hao baada ya kupewa shilingi 2,000.
Alisema aligundua hilo kufuatia
tabia ya mtoto wake kuchelewa kurudi nyumbani.
Naye Mbunge wa Arusha Mjini kwa
tiketi ya Chadema, Godbless Lema ambaye alifika hospitalini kuwajulia hali
watoto hao alisikitishwa na kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi lifanye
uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vipimo vya kidaktari ili kupata ukweli wa
tukio hilo.
“Nimeongea na mkuu wa mkoa, Magesa
Mulongo ambaye ameahidi kulifuatilia kwa kina suala hili na kujua undani
wake,’’ alisema Lema.
Hata hivyo, watoto hao baadaye
walihamishiwa katika Hospitali ya Seliani kwa ajili ya vipimo zaidi huku
taarifa za awali zikithibitishwa na daktari wa hospitali hiyo kuwa, baadhi yao
walikutwa na michubuko na kupanuka sehemu za siri hali inayooneshwa kuingiliwa.
Watuhumiwa wa tukio hilo
wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kwa uchunguzi zaidi
na Kamanda wa Polisi Arusha, Leberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments: