DIWANI WA CHADEMA ATUHUMIWA KUTOA RUSHWA NDANI YA
UCHAGUZI.
*Wajumbe wachapana makonde kavu kavu,Kahama.
UCHAGUZI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umeingia dosari,baada
ya mmoja wa madiwani wa chama hicho kuhusisha na rushwa na vitendo vya usaliti
ndani ya chama kutoka CCM.
Pia katika uchaguzi huo baadhi ya
wagombea wamechapana makonde huku baada ya kuenguliwa kwa baadhi ya majina ya
wagombea katika uchaguzi wa Baraza la Vijana wa chama hicho (BAVICHA),huku
Red Brigade wakihusika katika vurugu hizo.
Hali hiyo ilitokea jana mjini Kahama
katika ukumbi wa Mamba hali, baada mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama
hicho wilayani hapa Leonard Mayala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyasubi,
alienguliwa kuwania nafasi hiyo baada ya kubainika kutumia rushwa kuomba
achaguliwe katika nafasi hiyo.
Mgombea huyo alituhumiwa kutumia
shuilingi milioni mbili kuwahonga baadhi ya wanachama,fedha ambazo zinadaiwa
zilitolewa na baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi kwa njia ya mtandao wa
(Mpesa)ili kuhakisha ananyakuwa nafasi hiyo.
Tuhuma hizo zimekuja baada ya
wanachama kutokuwa na imani naye kutokana na mwenendo wa diwani huyo wa kuwa
karibu na makada wa CCM wilayani hapa na hivyo kusababisha viongozi na
wasimamizi wa uchaguzi huo kuengua jina lake baada ya kuridhika na
ushahidi uliotolewa na kuwekewa pingamizi.
Aidha katika uchaguzi huo baadhi ya
wagombea na wanachama walichapana makonde wakipinga kuenguliwa majina ya baadhi
majina ya wagombea katika uchaguzi wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA).
Ugomvi huo ulitokea baada ya
wagombea waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti wa Bavicha kuanza
kujinadi kwa wananchama ndipo mgombea Thomas Masanja aliyeenguliwa katika
kinyang’anyiro hicho kutokana na kukosa sifa ikiwemo kadi yake ya uanachana
kutotambulika alijitokeza na kuzuia uchaguzi.
Kufuatia kuenguliwa kwa mgombea huyo
ndipo badhi ya wafuasi wake wakiwemo Red Brigade walipojitokeza na
kuanza kufanya fujo kwa lengo la kuzuia uchaguzi huo kuendelea wakidai
kwamba mgombea wao kutotendewa haki kwa kuenguliwa kinyemela kugombea
nafasi hiyo.
Hali hiyo ilikwenda mbali zaidi
kwani wafuasi hao walianza kuwashambulia baadhi ya viongozi na
wasimamizi ambapo Mwenyekiti wa Chadema wa Halmashauri ya Msalala Emmanuel
Bombeda alipingwa ngumi na Red brigade waliokuwa wakimuunga mkono mgombea
aliyeenguliwa.
Utulivu na amani urejea ukumbini
humo baada ya msimamizi wa uchaguzi wa Chama hicho kanda ya Ziwa Mashairiki,Madata
Sande kuingilia kati na kuwataka wanachama kuwa wavumilivu ili
kufanikisha uchaguzi huo kwani wagombea walioenguliewa katika kinyang’anyiro
hicho walienguliwa kihalali bila upendeleo wowote kwa kuzingatia katiba
ya chama hicho.
Katika uchaguzi huo wajumbe
walimchagua Juma Protas,kuwa Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya hiyo,naye Mshibu
Peter akiteuliwa kushika nafasi ya Ukatibu wa chama hicho,nafasi ya Ukatibu Uenezi
ikimwangukia Anord Peter na Mweka Hazina alichaguliwa,Elias Mayunga.
Nalo Baraza la Vijana BAVICHA
lilimchagua Samwel Peter kuwa Mwenyekiti wake na ndani ya uchaguzi huo wajumbe
walichagua viongozi mbali mbali wa yakiwemo mabaraza ya Wazee,Wanawanake
na wajumbe wa mkutano mkuu taifa wa chama hicho.
Mwisho
No comments: