Meneja wa mazingira wa mkoa wa shinyanga mziray mwenye shati la mabaka akimuonyesha mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Rufunga hualibifu wa mazingira katika mistu wa mkweni wakati wa ziara yake ya siku tatu wilayani kahama .
Meneja mazingira mkoa wa shinyanga mziray akimuonyesha mkuu wa mkoa wa shinyanga mwenye suti nyeusi mpaka wa msitu wa mkweni na mpaka wa makazi ya wananchi.
Baadhi ya askali polisi na viongozi wa ulinzi na usalama wa mkoa wa shinyanga hakiaribu tanulul la mkaa katika msitu wa mkweni.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga wakiangali jinsi wanakijiji cha wendele walivyofanya uhabifu mkubwa ktika msitu wa mkweni kwa kuchana bao na kuchoma mkaa katika msitu huo .
Meneja wa mazingira mkoa wa shinyanga mziray akipatia maelenzo mkuu wa mkoa Ally Rufunga jinsi wanachi wanavyofanya uvamizi katika maeneo ya hifadhi kinyume na sheria za nchi .
Hivi ndiyo hali ilivyokuwa ya ukataji wa mistu katika hifadhi ya mkweni kama jinsi tulivyokuta mkaa umekwisha chomwa.
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Ally Rufunga Akihutubia wanakijiji wanaunzuka hifadhi ya mkweni ni marufuku kuingi katika hifadhi hiyo na kufanya shughuli za uchomaji mkaa na ukataji wa bao katika hifadhi hiyo .
KUAFUATIA
Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kuzuia ukataji wa miti katika ya Mbao katika
msitu wa Mkweni Wilayani Kahama kunaweza kusababisha ukosefu wa uji kwa
wanafunzi wa shule ya msingi Wendele kutokana na wazazi wao kutegemea shunguli
za ukataji haramu wa magogo ya mbao katika misitu huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alitoa tamko hilo la kuzuia shughuli za
ukataji wa miti haramu unaofanywa na
wanakijiji wa kijiji cha Wendele kilichopo jirani na Msitu huo kuingia katika
hifadhi na kusababisha uharibifu mkubwa wa ukataji wa miti ikiwa ni pamoja na
shughuli za uchomaji wa mkaa.
Katika
Ziara hiyo ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na
Mkuu huyo wa Mkoa ilishudia uharibifu ukubwa wa ukataji wa miti katika msitu
huo wa Mkweni ambao ndio pekee uliobaki katika Mkoa wa shinyanga huku wakazi wa
Kijiji cha Wendele wakifanya biashara ya magogo nyakati za usiku hali ambayo
inaashiria msitu huo kutoweka siku za baadaye.
Awali
Mwalimu wa shule ya Msingi Wendele Joyce Marungi akiuliza swali katika Mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho alisema kuwa uzuiwaji wa shughuli za
ukataji wa miti ya mbao katika msitu unaweza kuathiri wanafuni katika shule
kupata uji kwani wazazi wa kijiji hicho wanategemea kupata fedha kupitia msitu
huo.
Marungi
alisema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakifanya biashara ya mbao kuptia katika
msitu huo wa Mkweni na hivyo kujipatia fedha zinazopelekea kuwasadia katika
kulipia wanafunzi ada za shule pamoja na huduma ya kupata uji wanafunzi wawapo
mashuleni na hivyo kuongeza mahudhurio.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa shinyanga alipingana na mawazo hayo na kuongeza kuwa
jukumu za kulinda msitu kwanza ni la wananchi na kuongheza kuwa uharibifu wa
mazao ya misitu Serikali haiwezi kukubaliana nalo kwani linapoteza vyanzo vya
maji na upungufu wa mvua katika maeneo husika yaliopo jirani na hifadhi hiyo.
Aidha
Rufunga alisema kuwa kwa sasa Sheria zinatungwa na serikali itafanya mikutano
ya kuwaelimisha wananchi wa Vijiji 12 vinavyozunguka Msitu huo kuhusu faida ya
kuwa na misitu ili kuweza kuunuru Msitu huo ambo unaweza kutoweka kwa kasi
kulingana na ukataji wa mbao pamoja na shighuli za ukataji wa Mkaa.
Rufunga
aliwataka viongozi, Polisi, Sungusungu washiriki kwa pamoja katika
kuhakikisha msitu huo unalindwa na kuwataka wanakijiji wa kijiji cha Mkweni
kubuni shughuli nyingine ya kuwaingizia kipata na kuachana na kuingia msituni
kukata mbao hali ambayo Serikali haiwezi kukubaliana na uharaibifu wa msitu
huo.
Alisema
kuwa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkao ilifanya ziara ya ghafla katika Msitu
huo wenye ukubwa wa hekta 15744 kwa lengo la kukagua na kuona jinsi uharibifu
uliofanyuika katika msitu huo ikiwa ni pamoja na kuona ni jinsi gani ya kutunga
sheria ndogo itakayolinda hifadhi hiyo moja iliyobaki katika Mkoa wa Shinyanga
ili mkoa huo uweze kuepukana na jangwa.
mwisho
No comments: