Na Mohab Dominick
Kahama
Mwanamume mmoja ambaye hakufahamika majina wala makazi yake (40-45) ameuawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuhusika kumuuwa Asha Malale (60) mkazi wa kijiji cha Mbika kata ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha, tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tisa usiku muda mfupi baada ya bi, Asha Malale kuuawa kwa kukatwa na mapanga akiwa nyumbani kwake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za Kishirikina.
Alisema baada ya kutokea mauaji hayo ya bibi kizee, mjukuu wake Aitwaye Kafuku Shabani ambaye alikuwa akiishi naye alipiga kelele wakati mtuhumiwa akiwa bado yupo eneo la tukio, ndipo watu walifika na kuanza kumkimbiza na kumshambulia kwa kupiga mawe na kusababisha kifo chake na baadaye kumchoma moto.
Hata hivyo kamanda Kamugisha aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wawafikishe katika vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake kwani kuwaua watuhumiwa ni kupoteza ushahidi pamoja na kushindwa kuutambua mtandao wanaojihusisha na mauaji hayo.
“Kwa sasa tunaaendelea na uchunguzi wa matukio hayo huku wananchi tukiwataka kuonesha ushirikiano mkubwa katika kuwabaini wahusika wengine waliohusika kumuua Asha Malale” alisema kamanda Kamgisha.
Mwisho.
No comments: