Basi la Musoma Express lenye namba za usajili
T138 BDQ lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Musoma limepata ajali majira
ya saa 4 usiku katika kijiji cha
usanda shinyanga vijijini .
Basi hilo limepata ajali katika eneo la Usanda hatua chache baada ya kutoka katika mzani wa Tinde barabara ya Tinde Shinyanga.
Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamume mmoja anayedaiwa kuwa ni mzee (mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.
wakizungumza na mmoja wa askari wa jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga aliyeko katika eneo la tukio,ambaye hakutaka jina lake
litajwe kwa sababu yeye siyo msemaji, amesema mwanamume aliyegongwa na
gari hilo amefariki dunia papo hapo na kwamba abiria waliokuwa kwenye basi hilo
wako salama(hakuna majeruhi wala waliopoteza maisha).
Walioshuhudia tukio hilo wameiambia kuwa dereva wa basi hilo hakuwa katika mwendo
kasi ndiyo maana hakujatokea majanga zaidi.
Jeshi la polis limefika katika eneo la tukio na ,Kamanda wa polisi mkoa wa
shinyanga Justus kamugishi amedhibitisha
kutokea kwa ajali hiyo .na kusema ni mtu moja mtembea kwa miguu alipoteza maisha
hapo hapo.
No comments: