mkuuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya mwenye sharti la drafit akiwa na waadishi wa habari katika ukaguzi wa mahabara katika shule ya sekondari Bugish kuona ujenzi huo.
Dc mkuu wa wilaya ya kahama akitoa ufafanuzi juu ya ukamilishaji wa ujenzi wa mahabara na waandishi wa habari kahama .
Mtendaji wa kata ya nyasubi Mussa isango akimuonyesha mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya alijishika kiuno jinsi walipofikia katika Rita kwanye shule ya sekondari ya nyasubi jinsi wanachi walipofikia na mchango wao katika ujenzi huo wa mahabara .
Hivi ndiyo waandishi wa habari wilayani kahama walivyojitolea katika ujenzi wa mahabari katika shule za sekondari .
Mkuu wa wilaya ya kahama Benson mpesya akiwanga kokoto za zege .
ukanguzi wa mahabara katika shule ya sekondari ya nyasubi akiwa na waandishi wa habari .
mkuu wa wilaya akiwa amebeba ndoo ya mawe katika kushiriki katika ujenzi wa mahabara .
waandishi wa habari wakipewa taarifa na mtendaji wa kata ya nyasubi mussa ishago
muandishi wa gazeti la habarileo Raymond Mihayo akiwa katika moja ya ushiriki wa ujenzi wa mahabara katika shule ya nyasubi wilayani kahama.
mkuu wa wilaya akipewa tarifa za ufatuaji wa matofari ambapo kambi hiyo imewekwa katika ofisi za halmashauri ya mji wa kahama ambapo jumla ya matofari elfu 31 ambayo yapo tayari kwa ajili ya kupelekwa katika shule mbalimbali wilayani hapo ambapo lengo ni kufikisha tofari elf 40.
waandishi wa habari wakifanya kazi ya kuchota kokoto za ujenzi wa mahabara .
mkuu wa wilaya ya kahama akichota kokoto
Mwenyeki wa wandishi wa habari mkoa wa shinyanga shija
Felician katika shule ya sekondari ya bugisha
Mkuu wa wilaya kahama Benson mpesya akiwanga kokoto ya kuwanga zege .
Diwani ya kata ya mondo mh said akiangalia ufatuaji wa matofali
waandisha habari wakimsiliza mkuu wa wilaya ya kahama juu wa ujenzi wa mahabari .
Mtendaji wa kata ya nyasubi mussa ishago akiongea na waandishi wa habari juu ya ujenzi wa mahabara ktikati kata ya nyasubi.
Hivi ndiyo ujenzi umefikia katika Rita shule ya sekondari nyasubi .
Dc karibu sana mh diwani hayo ndiyo maneno ya dc mpesya kwa diwani wa kata ya mondo katika kumpongeza kwa kukamilishaji wake wa jengo la mahabara katika kata yake .
Meona kazi yetu waandishi wa habari hayo ni maneno ya Dc mpesya
Hapa ni kazi tu waandishi wa habari .
Mkuu wa wilaya ya kahama akisitiza jambo la ujenzi wa mahabari kwa waandishi wa habari ofisini kwake .
Mafundi wakiendelea na kazi .
DC mpesya na waandishi wahabari pichani ofisini kwake.
Mkuu haya ndiyo matofari Elf 31 ambapo fundi mkuu wa ufatuaji wa matofali juma ally alisema kuwa lengo ni matofali Elf 40 ambapo tayari yapo ni Elf 31.
Haya ndiyo matofari yalipo tayari kwa ujenzi huo wa mahabara .
Hapa ni kazi tu kwa waandishi wa habari .
Waandishi wa Habari Wilayani Kahama jana wameshiriki katika
shughuli ya ujenzi wa vyumba vya maabara ya shule za sekondari katika azma ya
kuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Waandishi hao wa
habari walioongozwa na mwenyekiti wa
chama cha waandishi wa habari mkoaani humo (SPC) ,Shija Felician ,walikuwa bega
kwa bega na Mkuu wa wilaya ya Kahama
Benson Mpesya katika mradi wa ujenzi huo Shule ya Sekondari Nyasubi ,mjini Kahama
jana.
Mwenyekiti huyo wa SPC
mkoani Shinyanga alimwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa lengo la kushiriki ujenzi
huo ni kumuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwani manufaa ya mpango huo ni
makubwa kwa taifa na haupaswi kubezwa au kupuuuzwa na mtu yeyote wala chama
chochote cha siasa.
“Taifa haliwezi kutegemea wanasayansi,wataalamu kutoka nje ya
nchi hivyo lazima juhudi za lazima zifanywe kujenga maabara katika shule zote
nchini,kuongeza vitabu vya masomo ya fizikia,kemia ,baolojia na hisabati ili
maabara hizo zilete tija.”Alisema Felician.
Mpesya aliwashukuru wanahabari hao kwa kujitolea katika
kufanikisha mpango huo kwa vitendo na kutaka wanajamii wengine kuiga mfano huo.
Naye Mkuu huyo wa wilaya alisema wameweza kufyatua matofali
31,000 hadi sasa kati ya lengo la matofali
41,000 kwa msaada wa wafanyabiashara,taasisi za umma na binafsi na
migodi ya Dhahabu ya Buzwagi na Bulyankulu.
Alisema kazi ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika
halmashauri za Ushetu,Msalala na Mji wa Kahama inaendelea vizuri na
anamatumaini ya kukamilisha kabla ya muda uliowekwa na Rais wa Jamhuri mjini
Dodoma mwaka jana na kusisitizwa tena
hivi karibun.i
Kwa mfano alifafanua,Halmashauri ya Ushetu ilipanga kuwa na
vyumba 45 vya maabara,katika hivyo 21 vimekaribia kukamilika na 20 vinaendelea kujengwa na vinne katika hatua za mwisho.Halmashauri ya
Msalala lengo ni vyumba 42,17 vimekamilika 23 vinajengwa na viwili vinatumika.
Halmashauri ya mji wa Kahama ,lengo ni vyumba 42,vitano
vinafanya kazi, 37 viko katika hatua mbalimbali za ujenzi na vitakamilika kabla
ya Novemba 30,mwaka huu.
Mratibu wa mradi huo Agnes Kahezela alifafanua kuwa baada ya
kufyatuliwa matofali hayo hupelekwa moja kwa moja saiti kuendeleza shughuli za
ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara za sekondari wilayani humo.
Mwisho
No comments: