sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Kimataifa Habari

habari

Habari Za Mastaa

Michezo

simulizi za kusisimua

» » » MBOGWE YAPITISHA BAJETI- 2015/2016 ZAIDI YA BIL 30
MBOGWE
 BARAZA la Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita leo imepitisha Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016 kiasi cha  zaidi ya shilingi Bil 30.363 huku ikijikita kukusanya  mapato katika vyanzo vyake mbalimbali vya ndani na kupunguza utegemezi toka serikali kuu.

Baada ya mapitio ya bajeti hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbogwe mh Vicent Busiga halmashauri kwa mwaka 2015/2016 inakusudia kupokea kukusanya fedha hizo kutoka vyanzo mbalimbali kama vile mishahara ,mapato ya ndani ,utawala Ruzuku ya utawala (GPG)Mifuko mbalimbali ya maendeleo na matumizi mengine.

Busiga amesema mikakati mitano ambayo Halmashauri hiyo imejiwekea ili kufikia lengo ni ubinafsishaji vyanzo vya mapato vya halmashauri,na
kuanza kutoa vyanzo vipya mara baada ya sheria ya halmashauri ya
wilaya kuidhinishwa na waziri mwenye dhamana.

Amesema mikakati mingine ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kubuni mikakati mbalimbali ambayo itaboresha makusanyo na kuendelea kuibua vyanzo vipya ambavyo havitegemei hali ya hewa na vinavyohitaji gharama kidogo za makusanyo.
Aidha Busiga amesema Halmashauri itaendelea kutoa mafunzo mbalimbali ambayo yataboresha utekelezaji wa Bajeti kwa mfano utawala bora na utunzaji wa Raslimali za Uma.

Baada ya kauli moja ya kukubali kupitisha Bajeti hiyo mwenyekiti  wa
halamshauri mh Busiga amewataka madiwani ,watendaji  wahakikishe
wanasimamia mpango mkakati waliojiwekea ili kuweza kukusanya mapato kutokana na vyanzo vya ndani ili kuepuka ama kupunguza  utegemezi hali ambayo imekuwa ikiifanya halmashauri hiyo kutokukamilisha miradi kutokana na wategemewa kupeleka fedha kwa muda ambao wao wanapenda.


«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply