Kwa
mujibu wa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama tawala cha Tanzania chama cha
Mapinduzi Nape Nnauye Mbunge huyo ambaye alikuwa maarufu kwa utunzi na uimbaji
wa nyimbo za kampeni za chama hicho kifo cha chake kimetokea siku ya jumamosi
majira ya jioni.
Marehemu
Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko
nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule
ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka
1974.
Mwaka
1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo
Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu
John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo
cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi
mwaka 1978.
Keptain
John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton
International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
No comments: