Baadhi ya wazee wa kijiwe cha kahawa wakiwa katika msangao baada ya wazee wenzao kuchukua fedha hizo za kahawa .
Hapa ndiyo eneo la kijiwe cha kahawa wakiwa wanasubiri kunywa kahawa.
Wazee wakinywa kahawa huku wakijadili jinsi gani hawa wazee wenzao ili kulipa fedha hizo.
Mmoja wa wazee akiwa ameshika mpini wa shoka ambapo moja wao baada ya mgao wa shilingi elfu kumi.
Hiki ni kijiwe cha kahawa bukombe alimarufu( chadema )
Mfanyabishara Kyanyari Daeil alitoa fedha za kunywa kahawa shilingi laki moja ili wazee watumie kwa mwezi moja.
Mwenye kibarakashia Abdallah Hamisi akingawa kahawa ambapo ni eneo la jirani yake Kyanyari
BUKOMBE
Mmoja wa mfanyabiashara wilayani bukombe mkoani Geita Daeil
kyanyari amecha vurungu kubwa katika kijiwe cha kahawa maarufu kwa jina la
kijiwe cha chadema kwa kukadhiwa muuza kahawa laki moja kwa ajili ya wateja
wake kunywa kwa mwezi moja.
Akiongea kwa masikitiko makubwa mumiliki wa kijiwe hicho
Abdalla Hamisi alisema kuwa huyo jamaa ni jirani yangu tu alifika hapa
kwakuwa na ofisi hapa karibu na kijiwe
hichi,aliona ni vyema kuwanunulia wazee kahawa,lakini hali hiyo iligeuka na
baadhi ya wazee walianza kungawana fedha hizo badala ya kupatie mwenye kijiwe
fedha hizo .
Moja ya wazee waliokuwepo hapo makonye masanja alisema kuwa
kitendo kilichofanywa na baadhi ya wazee hawa ni wizi kwa kuwa mwenye kijiwe
hicho halikuwa amekwenda kutafuta chenji kwa ajili ya wateja wake walikuwa
wanakunywa kahawa hapa.
“Hunajua huyu jamaa mwenye kutoa hizo fedha alifika hapo na
muuza kahawa yuko wapi?alijibiwa kuwa amekwenda kutafuta cheji ya wateja wake,ndipo
alitoa kiasi cha laki moja kwa ajili ya kunywa kwa mwezi moja tu alisema
makonye masanja.’’
Aidha Abdalla aliwataja wazee waliokuwepo
wakati wa kupokea fedha hizo na kuzingawa kwa pamoja aliwataja kwa majina yao
moja moja kuwa ni Richard,kabote ,lena bank ,Bujumbula ,kijana wa mwalo,mzee wa
Baiskeli ,mwingulu ,Juli mtusi ,na mgambo.akisimili hali hiyo Abdalla alisema
kuwa mimi mwenye sikuamini kuwa hawa wazee wagefanya hiyo.
Nipashe ilifuta muhusika wa kutoa fedha hizo ili kupata
ukweli wa jambo hilo naye alikuwa ha haya ya kusema kuwa huyu ni jirani yangu
Abdalla niliona ni vema nikawapa wazee hela kwa ajili ya kunywa kahawa kama
jirani yangu.
“mimi hapa ni jirani yangu nilichokifanya hapa ni upendo tu
kama mungu alisema mpende jirani yako kama nafsi yako na mimi kwa kuwa hapa ni
mgeni niliona ni vema kutoa fedha hiyo kiasi cha laki moja kwa mwenyeji wangu
hapa na alipokea hapa na kutoa fedha hizo ili wazee wanywe kwa mwezi moja
alisema kyanyari Daeil.’’
Aidha kanyari alisema sikuwa na nia mbaya kwa wazee wangu wao
walifanya makosa tu ya kushindwa kumpa fedha hizo Abdalla na wao kunywa tu
kahawa hizo kwa mwezi moja huo na sivingine alisema Daeil kanyayari kwa uzuni
sana.
Mwisho
No comments: