NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi
ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua
za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani
mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi,
Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha
Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya
kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka jana nilipofanya ziara
kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa
magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna
mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,”
alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi
ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya
kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni mara baada ya ukaguzi wa
kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa
aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
Akiwa mjini Chalinze, Masauni
alizungumza na waendesha bodaboda na kuwapa maelekezo kuhakikisha wanafuata
sheria za usalama barabarani kwa kutobeba mishikaki, uvaaji wa kofia ngumu na
pia kufuata sharia zote za usalama barabarani.
“Mmenihakikishia kwa wale ambao
hamkua na kofia ngumu kuwa mkitoka hapa mtakwenda kuzitafuta, hakikisheni
mnafanya hivyo kwa usalama wenu pamoja na abiria mnaowabeba, ipendeni kazi yenu
kwa kuheshimu sharia za usalama barabarani,” alisema Masauni.
Akiwa njiani kuelekea Chalinze mpaka
Bagamoyo, Masauni ambaye gari yake ilitolewa namba zinazomtambulisha nafasi
yake (NWMNN), na kuweka namba za kawaida ili kujua kama akiendesha kwa
mwendokasi barabarani matrafiki watalisimamisha gari lake, hata hivyo askari wa
usalama barabarani sehemu kubwa hawakuwepo barabarani na pia waliokuwepo
hawakuweza lisimamisha gari lake.
Kutokana na hatua hiyo, Masauni
akagundua kuwa kuna uzembe mkubwa unaofanywa na matrafiki mkoani humo kwa
kutofanyakazi zao kwa umakini, na kwa uzembe huo ndio chanzo cha ajali
zinazotokea barabarani mara kwa mara.
Akizungumza na matrafiki wilayani
Bagamoyo ambao walifanya uzembe huo, aliwataka wabadilike haraka iwezekanavyo
kufuata wajibu wao, na pia alitoa siku tatu kuhakikisha wanawakamata waendesha
bodaboda wote ambao wanavunja sheria za usalama barabarani, na pia baada ya
operesheni hiyo apewe ripoti haraka iwezekanavyo, na muda wowote atafanya ziara
ya kushtukiza kuona kama maelekezo hayo wameyafanyia kazi.
“Bodaboda nimeziona nyingi
zinapita hapa zikiwa zinavunja sheria, madereva na abiria hawajavaa kofia
ngumu, na nyie mpo hapa mnaziangalia, sasa nawaagiza mtekeleze maagizo
niliyotoa na pia sio nyie tu bali nchi nzima wahakikishe wanayakagua magari
pamoja na bodaboda, na atakaepuuza atutacheka nae, tutapambana nae,” alisema
Masauni.
Kwa upande wake Kamanda Msilimu,
alisema ameyapokea maagizo yote na atahakikisha anayafanyia kazi ipasavyo kwa
kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini mkubwa NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya

kuwasimamia matrafiki wote nchini kwa umakini mkubwa Kwa hisani ya Felix Mwagara (MOHA)
No comments: