Gari la maji ya kuwasha likiwa mtaani
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wilaya ya Shinyanga mjini kimesema kimefanikiwa kufanya
maandamano yao ya amani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu 2015
yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kupitia askari wa jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na Malunde1 blog mapema leo katibu wa Chadema wilaya ya Shinyanga mjini George Kitalama amesema wamefanikiwa kufanya maandamano yao kupitia jeshi la polisi akidai kuwa polisi wameandamana badala ya Chadema wakiwa na magari yao mtaani.
Amesema walipanga kufanya maandamano leo Novemba 03,2015 mji mzima wa Shinyanga lakini polisi ndiyo wamejitokeza kufanya maandamano wakiwa na magari yao kila mtaa.
Amesema tangu Novemba 02,2015 hadi leo Novemba 03,2015 misururu ya magari ya polisi yakiwemo ya maji ya kuwasha yakiwa na askari polisi yamekuwa yakiranda randa mtaani hivyo hiyo ni ishara tosha kuwa polisi wanaandamana kwa niaba ya Chadema.
Kitalama amesema Chadema wamefanikisha maandamano yao kupitia jeshi la polisi na magari yao mtaani hivyo kufikisha ujumbe kuwa Chadema haikubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments: