Mamlaka
ya anga ya Serikali ya Zimbabwe February 15 imetangaza kuikamata ndege
ya kimarekani inayomilikiwa na Western Global Airlines iliyokuwa imeomba
kutua kwa dharura katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare. Zimbabwe
imekamata ndege hiyo iliyokuwa inatoka Ujerumani ikiwa imebeba hela za
Afrika Kusini (rand) na maiti.
Ndege
hiyo ya mizigo aina ya MD11 iliomba kutua kwa dharura Harare ili ipate
msaada wa usalama, lakini ilikuwa inaenda Afrika Kusini na ilitua
Zimbabwe ili kuomba msaada wa mafuta kabla ya kuendelea na safari yao ya
Afrika Kusini. Uchunguzi wa ndege hiyo ulikuwa unaendelea.
Meneja
wa mamlaka ya anga ya Zimbabwe David Chaota amethibitisha kukamatwa kwa
ndege hiyo ya kampuni ya Western Global Airlines, kampuni ambayo ipo
Florida Marekani, inaripotiwa kuwa ilianza kuomba kutua Msumbiji lakini
ilikataliwa.
Chanzo-Millardayo.com
No comments: