RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA JOHN MPOMBE MAGUFULI | . |
Tanzania
inatarajiwa kusajili kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa uchumi wake mwaka huu
katika kanda ya Afrika Mashariki na kati.
Hii
ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha la kimataifa - IMF.
Katika
ripoti yake iliyotolewa nchini Tanzania inatarajiwa kusajili kiwango cha juu
cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa 2016.
Kasi
hiyo ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni ya pili tu nyuma ya Ivory Coast baina
ya mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara .
Image caption Tanzania inatarajiwa
kusajili kiwango cha juu cha ukuaji wa uchumi wake wa asilimia 6.9% mwaka wa
2016.
Ivory
Coast inatarajiwa kukuwa kwa kasi ya asilimia 8.5%.
Katika
kanda ya Afrika Mashariki ,uchumi wa Kenya ndio wa pili kwa kasi ya ukuaji kwa
asilimia 6%.
IMF
hata hivyo inasema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi kusini mwa jangwa la Sahara
unatarajiwa kupungua kwa mwaka wa pili mfululizo kutokana na kudorora kwa
viwango vya uzalishaji na hivyo uwekezaji.
Kwa
mujibu wa shirika la fedha la kimataifa - IMF, eneo hilo linakadiria kushuka
kwa ukuwaji wa uchumi kwa asilimia 3 mwaka huu.
Kiwango
hicho ni cha chini kabisa kuwahi kushuhudiwa katika miaka 15.
Mataifa
yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile
Nigeria na Angola.
Mataifa
yanayotegemea mapato yanayotokana na mafuta ndiyo yalioathirika zaidi kama vile
Nigeria na Angola.
Aidha
Zambia pia imeathirika vibaya kutokana na ukosefu wa soko la kimataifa la shaba
yake.
Ripoti
hiyo inaitaja Afrika Kusini kama moja ya mataifa ambayo kiwango chake cha
ukuaji kimedorora kwa kiasi kikubwa mno.
Katika
orodha ya mataifa yanayotarajiwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji Kusini mwa
jangwa la sahara Ivory Coast ndio inayoongoza.
Orodha ya mataifa ya kanda ya Kusini
mwa Jangwa la Sahara na viwango vya kasi ya ukuaji wa uchumi 2016.
1.
Ivory
Coast 8.5%
2.
Tanzania
6.9%
3.
Senegal
6.6%
4.
Kenya 6%
5.
Zambia
3.4%
6.
Nigeria
2.3%
7.
Afrika
Kusini 0.6%
No comments: